-
SanamuKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Kuhusu desturi ya Kanisa Katoliki, New Catholic Encyclopedia (1967, Buku la 7, uku. 372) husema hivi: “Kwa kuwa mtu anapoabudu sanamu huwa anamwabudu mtu anayewakilishwa na sanamu hiyo, vivyo hivyo ibada anayostahili mtu huyo inaweza kutolewa kwa sanamu inayomwakilisha.”
-
-
SanamuKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Je, wanaotumia sanamu humwabudu mtu anayewakilishwa, au baadhi ya sanamu huonwa kuwa muhimu kuliko nyingine?
Ni muhimu kufikiria maoni ya waabudu. Kwa nini? Jinsi ambavyo sanamu hutumiwa ndiyo huamua iwapo ni ibada ya sanamu au la.
Akilini mwa mwenye kuabudu, je, sanamu moja ya mtu fulani ni muhimu kuliko sanamu nyingine ya mtu huyohuyo? Ikiwa ndivyo, sanamu hiyo ndiyo inayoabudiwa, wala si mtu anayewakilishwa. Kwa nini watu hufunga safari ndefu kwenda kuabudu katika mahekalu hususa? Je, sanamu zenyewe sizo zinazoonwa kuwa na nguvu za “kimwujiza”? Kwa mfano, katika kitabu Les Trois Notre-Dame de la Cathédrale de Chartres, cha mtawa Yves Delaporte, tunaambiwa hivi kuhusu sanamu za Maria katika kanisa kuu huko Chartres, Ufaransa: “Sanamu hizo, zilizochongwa, zilizochorwa au zinazoonekana katika madirisha ya vioo vyenye rangi mbalimbali, hazilingani kwa umaarufu. . . . Sanamu tatu tu ndizo huabudiwa hasa: Our Lady of the Crypt, Our Lady of the Pillar, na Our Lady of the ‘Belle Verriere.’” Lakini ikiwa waabudu wangekuwa wakimwabudu hasa mtu anayewakilishwa na sanamu hizo, hakungekuwa na tofauti yoyote kati ya sanamu hizo, sivyo?
-