Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu
    Amkeni!—2007 | Machi
    • Jambo Linalozidi Kuhangaisha Jamii

      Tatizo hilo lilisababisha Idara ya Sheria na Usalama wa Umma huko New Jersey, Marekani, kuwatumia wazazi na walezi barua iliyokuwa na himizo hili: “Tusaidieni kukabiliana na tatizo linalozuka la matumizi yasiyofaa ya Intaneti miongoni mwa watoto wakiwa ndani au nje ya shule.” Barua hiyo ilieleza waziwazi hangaiko la idara hiyo kuhusu kuweka habari za kibinafsi na picha kwenye Intaneti. Vituo vinavyotoa habari kama hizo huwavutia walaghai wawe vijana au watu wazima. Barua hiyo ilisema hivi pia, “Wazazi mnapaswa kujua kwamba mahangaiko haya ni ya kweli na mnaweza kuchangia sana kuwalinda watoto wenu kwa kujifunza mengi kuhusu Intaneti na kujua vituo ambavyo watoto wenu hufungua.”

      Hata hivyo, wazazi wengine wanajua machache sana kuhusu yale ambayo watoto wao wanafanya kwenye Intaneti. Mama mmoja ambaye hufuatilia kwa ukaribu kile ambacho binti yake mwenye umri wa miaka 16 anafanya kwenye Intaneti anasema hivi: “Wazazi wanaweza kushtuka na kuaibika sana wakijua mambo ambayo watoto wao huweka na kuzungumzia kwenye Intaneti.” Kulingana na mtaalamu mmoja wa usalama kwenye Intaneti, vijana fulani huweka picha walizopigwa wakiwa wamevalia vibaya.

      Madhara

      Je, malalamiko hayo yanatoka kwa watu wazima wenye wasiwasi mwingi ambao wamesahau vituko vyao vya ujanani? Takwimu zinaonyesha hilo si kweli. Fikiria hili: Katika maeneo fulani, karibu asilimia 33 hivi ya wavulana na wasichana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 17 wamewahi kufanya ngono. Zaidi ya nusu ya vijana wenye miaka kati ya 13 na 19 wanasema kwamba wamefanya ngono ya kinywa.

      Je, teknolojia imechangia takwimu hizo zenye kushtua? Bila shaka. Ripoti moja katika gazeti New York Times Magazine inasema kwamba “simu za mkononi na Intaneti, ambazo huwawezesha vijana kufanya mambo bila kujulikana, hufanya iwe rahisi kwao kukutana na kufanya ngono bila kuwajibika.” Kwa kweli, inachukua muda mfupi sana kwenye kompyuta kupanga kukutana kwa siri na mtu wa jinsia nyingine. Katika uchunguzi mmoja, zaidi ya wasichana 4 kati ya 5 walikiri kwamba hawawi waangalifu sana wanapotumia Intaneti.

      Watu wengine wanaotafuta mchumba au mtu wa kufanya naye ngono bila kuwajibika wamepata zaidi ya yale waliyotarajia. ‘Tumeshuhudia ongezeko la visa vya watu kulalwa kwa nguvu,’ anasema Jennifer Welch wa Idara ya Polisi ya Novato huko California. Anasema kwamba wahasiriwa wengi huwa wamewasiliana kwanza kupitia Intaneti na kukubali kukutana na watu ambao baadaye huwadhulumu.

      Jihadhari na “Hekima ya Ulimwengu”!

      Makala ya kuwashauri vijana katika magazeti hayachukui msimamo thabiti inapohusu vijana na ngono. Ingawa wanawatia moyo vijana kuwa safi kiadili au kujiepusha na ngono, lengo lao kuu ni kuwatia moyo wajihusishe na ngono “salama” badala ya kutojihusisha hata kidogo na ngono. Ni kama wanasema hivi: ‘Hatuwezi kuwazuia lakini angalau tunaweza kuwafundisha wawajibike.’

      Kwenye makala iliyotolewa kwenye kituo kimoja cha Intaneti kinachoheshimika ambacho hutoa ushauri kwa vijana, suala la ama mtu anapaswa au hapaswi kufanya ngono lilitegemea mambo matatu: (1) hatari za kupata mimba, (2) hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na (3) umuhimu wa kuamua kama msichana na mvulana wako tayari kihisia kufanya jambo hilo. “Lakini wewe ndiye utakayefanya uamuzi wa mwisho,” kinasema kituo hicho. Kilitaja kijuujuu tu kwamba mtu anapaswa pia kuzungumzia jambo hilo pamoja na mzazi wake. Makala hiyo haikutaja kama ni sawa ama si sawa kwa vijana kufanya ngono.

      Ikiwa wewe ni mzazi, bila shaka ungependa watoto wako waongozwe na maoni bora zaidi kuliko “hekima ya ulimwengu” ambayo ni ya kipumbavu. (1 Wakorintho 1:20) Unaweza kuwasaidiaje wapite kipindi cha kubalehe na kuepuka hatari zilizozungumziwa katika makala hii? Jibu haliwezi kuwa tu kufunga kompyuta au kuwanyang’anya simu. Kusuluhisha mambo kijuujuu hakugusi mioyo. (Methali 4:23) Kumbuka pia kwamba huenda watoto wakawa wanatumia vifaa kama simu na Intaneti kutosheleza mahitaji fulani ambayo ukiwa mzazi unaweza kuyatosheleza kwa njia bora. Ni nini baadhi ya mahitaji hayo?

  • Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu
    Amkeni!—2007 | Machi
    • a Badala ya wazazi kushutumu Intaneti, wanapaswa kujua vituo ambavyo watoto wao hupenda kuvifungua. Kwa njia hiyo, watoto wanaweza kusaidiwa ‘kuzoeza nguvu zao za ufahamu kutofautisha yaliyo sawa na yaliyo makosa pia.’ (Waebrania 5:14) Mazoezi kama hayo kutoka kwa wazazi yatawasaidia watoto wanapokomaa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki