-
Jinsi Wainka Walivyopoteza Milki Yao Yenye FahariAmkeni!—1998 | Januari 8
-
-
Polepole, miale ya jua ilifika chini na kuangaza hekalu la jua lililo katikati ya jiji kuu la Milki ya Inka, Cuzco (limaanishalo “Kitovu cha Ulimwengu”). Kuta zenye dhahabu ziliangaza miale ya jua. Michongo ya dhahabu tupu ya Ilama, vicuñas, na tai iling’aa katika bustani ya Wainkaa iliyokuwa mbele ya hekalu.
-
-
Jinsi Wainka Walivyopoteza Milki Yao Yenye FahariAmkeni!—1998 | Januari 8
-
-
Wainka walijua sana kujenga majengo makubwa. Kuna mawazo mengi kuhusu jinsi wasanifuujenzi wao walivyoweza kujenga ngome na hekalu la Sacsahuaman, ambalo laonekana sana katika jiji la Cuzco kutoka uwanda wa juu. Majabali makubwa mno yenye uzito wa tani 100 yaliunganishwa pamoja. Hakuna mota iliyotumiwa kuyashikanisha. Matetemeko ya ardhi hayajaathiri sana mawe hayo yaliyounganishwa vizuri sana katika kuta za jiji la kale la Cuzco.
Hekalu Lenye Kung’aa la Jua
Katika jiji la kifalme la Cuzco, Wainka walipanga ukuhani kwa ajili ya kuabudu jua katika hekalu la mawe lililong’arishwa. Kuta za ndani zilipambwa kwa dhahabu safi na fedha.
-