Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unaweza Kukabiliana na Ukosefu wa Haki!
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Agosti 15
    • Mtu mwingine aliyetendewa isivyo haki ni Nabothi. Yezebeli, mke wa Mfalme Ahabu wa Israeli alipanga njama ya hila juu yake. Mfalme alitamani shamba la urithi la Nabothi ambalo lilikuwa kando ya jumba la mfalme. Mwisraeli hakupaswa kumpa mtu mwingine shamba lake la urithi, hivyo Nabothi alikataa kumuuzia mfalme shamba hilo. (Mambo ya Walawi 25:23) Basi, mke mwovu wa Ahabu alipanga mashahidi wa uwongo wamshtaki Nabothi kwa kudai kwamba amemkufuru Mungu na kumlaani mfalme. Kwa sababu hiyo, Nabothi na wanawe waliuawa. Hebu wazia jinsi Nabothi alivyohisi watu walipokuwa wakiokota mawe ili wamuue!—1 Wafalme 21:1-14; 2 Wafalme 9:26.

  • Unaweza Kukabiliana na Ukosefu wa Haki!
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Agosti 15
    • Namna gani Nabothi? Jaribu tena kuona jambo hilo kama Yehova alivyoliona. Machoni pa Yehova, ambaye anaweza kuwafufua wafu, ni kana kwamba Nabothi alikuwa hai ingawa alikuwa maiti. (1 Wafalme 21:19; Luka 20:37, 38) Nabothi hana budi kungoja mpaka wakati ambapo Yehova atamfufua, lakini muda huo ni mfupi tu, kwa kuwa wafu hawajui lolote kamwe. (Mhubiri 9:5) Zaidi ya hilo, Yehova alimlipizia kisasi Nabothi kwa kumhukumu Ahabu na watu wa nyumba yake.—2 Wafalme 9:21, 24, 26, 35, 36; 10:1-11; Yohana 5:28, 29.

  • Unaweza Kukabiliana na Ukosefu wa Haki!
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Agosti 15
    • [Picha katika ukurasa wa 16, 17]

      Nabothi alihisi namna gani alipotendewa isivyo haki?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki