Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wenye Kubadilikana, Hata Hivyo Wenye Wajibu Kuelekea Viwango vya Kimungu
    Amkeni!—1997 | Januari 22
    • Uhusiano Imara Pamoja na Yehova

      Ukosefu wa ustahimilivu hutokea katika mazingira ya hangaiko. Hata hivyo, ikiwa tuna uhusiano wa karibu pamoja na Mungu, sisi hufurahia hisi ya usalama ambayo hutusaidia kudumisha usawaziko ufaao. “Jina la BWANA ni ngome imara; mwenye haki huikimbilia akawa salama,” ndivyo tusomavyo kwenye Mithali 18:10. Kwa hakika hakuna madhara yawezayo kutupata au kupata wapendwa wetu ambayo Muumba hatayashughulikia kwa wakati wake.

      Mtu aliyenufaika sana kutokana na uhusiano mzuri pamoja na Mungu alikuwa mtume Paulo. Akiwa Myahudi aliyeitwa Sauli, yeye aliwanyanyasa wafuasi wa Yesu Kristo na alikuwa na hatia ya umwagaji wa damu. Lakini Sauli mwenyewe alikuja kuwa Mkristo, na akiwa mtume Paulo, baadaye alieneza evanjeli kwa wakati wote. Paulo alidhihirisha mtazamo wa akili iliyofunguka kwa kuhubiria watu wote, “kwa Wagiriki na kwa Wabaribari pia, kwa wenye hekima na kwa wasio na akili pia.”—Waroma 1:14, 15; Matendo 8:1-3.

      Yeye alifauluje kubadilika? Kwa kupata ujuzi sahihi wa Maandiko na kukua katika upendo kwa Muumba, ambaye hana upendeleo. Paulo alijifunza kwamba Mungu ni mwenye haki katika njia ya kwamba Yeye huhukumu watu wakiwa mtu mmoja-mmoja, si kulingana na utamaduni au jamii, lakini kulingana na kile alicho mtu na anachofanya. Ndiyo, kwa Mungu, matendo ni ya muhimu. Petro alitaja kwamba “Mungu si mwenye ubaguzi, bali katika kila taifa mtu ambaye humhofu na kutenda uadilifu akubalika kwake.” (Matendo 10:34, 35) Mungu Mweza Yote hana upendeleo. Ni tofauti na viongozi fulani wa ulimwengu, ambao huenda wakatumia ukosefu wa ustahimilivu kimakusudi kwa makusudi yao wenyewe.

  • Wenye Kubadilikana, Hata Hivyo Wenye Wajibu Kuelekea Viwango vya Kimungu
    Amkeni!—1997 | Januari 22
    • Theofano, mwanafunzi Mgiriki, aliyeeleza kwamba wakati uliotumiwa pamoja na watu wa malezi tofauti-tofauti uliongoza katika kuwafahamu vizuri zaidi, alisema: “Ni jambo la muhimu kwamba tujaribu kuona jinsi wanavyofikiri badala ya kuwalazimisha kufuata njia yetu ya kufikiri.”Kwa hiyo, kwa kupata kumjua mtu vyema zaidi, twaweza kugundua kwamba ladha yake katika chakula na hata lahaja yake si ya ajabu kama tulivyofikiri. Badala ya nyakati zote kuwa na mengi ya kusema kuliko wengine au kusisitiza kusema neno la mwisho, twajifunza mambo yenye mafaa kwa kusikiliza maoni ya mwingine. Kwa hakika, watu wenye akili iliyofunguka hupata maisha yakiwa yenye kuthawabisha sana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki