Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ripoti ya Ulimwenguni Pote
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Tahiti

      Makemo ni kisiwa kidogo cha matumbawe kilicho umbali wa kilomita 600 kutoka Tahiti na kina wakaaji 720. Mwanamke mmoja aitwaye Ravahere alijua kweli kwa kadiri fulani alipokuwa akikaa na watu wa jamaa yake kisiwani Tahiti. Aliporudi Makemo, alianza kujifunza Biblia kupitia barua, kisha faksi, na baadaye simu. Ravahere alihalalisha ndoa yake na kufanya mabadiliko mengine ili aishi kupatana na viwango vya Yehova. Alifanya hivyo licha ya mkazo kutoka kwa baadhi ya watu wa familia yao ambao hawakutaka aache dini ya Mormon. Mwishowe, Ravahere alistahili kuwa mhubiri ambaye hajabatizwa alipotembelea kutaniko fulani huko Tahiti. Anapokea barua kutoka kwa wahubiri wengine katika kutaniko hilo kila baada ya majuma mawili.

      Mnamo Juni 2006, mwangalizi wa mzunguko na mke wake walimtembelea Ravahere. Mwangalizi huyo alieleza kwamba Ravahere huhubiri nyumba kwa nyumba kila Jumamosi na Jumapili. Amechora ramani ya eneo lake na ameanzisha mafunzo kadhaa ya Biblia. Yeye huweka magazeti yetu kwenye duka lake dogo, mahali ambapo watu wanaweza kuyaona. Pia anaongoza funzo la kitabu, na mume wake huhudhuria.

  • Ripoti ya Ulimwenguni Pote
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 63]

      Ravahere akiwa katika duka lake dogo huko Makemo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki