Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Makasisi Wawili Waliothamini Vitabu vya Russell
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Aprili 15
    • Makasisi Wawili Waliothamini Vitabu vya Russell

      KATIKA mwaka wa 1891, Charles Taze Russell, aliyefanya kazi kubwa sana miongoni mwa waabudu wa kweli wa Yehova, alizuru Ulaya kwa mara ya kwanza. Kulingana na ripoti fulani, alipofika Pinerolo, Italia, Russell alikutana na Profesa Daniele Rivoire, aliyekuwa kasisi wa dini ya Wawaldo.a Ingawa Rivoire aliendelea kushirikiana kwa ukaribu na Wawaldo baada ya kuacha ukasisi, alikuwa tayari kujifunza mambo mapya na alisoma vichapo vingi vilivyoandikwa na C. T. Russell.

      Katika mwaka wa 1903, Rivoire alitafsiri kitabu cha Russell The Divine Plan of the Ages katika Kiitalia na kulipia gharama za uchapishaji. Hii ilikuwa kabla Mashahidi wa Yehova hawajachapisha kitabu hicho katika Kiitalia. Katika dibaji ya kitabu hicho, Rivoire aliandika hivi: “Twaacha tafsiri hii ya kwanza ya Kiitalia chini ya ulinzi wa Bwana. Na aibariki licha ya makosa yaliyomo ili ichangie kutukuzwa kwa jina lake lililo takatifu sana na kufanya watoto wake wanaozungumza Kiitalia wajitoe kabisa kwa Mungu. Wote ambao kwa kusoma kitabu hiki wanathamini kina cha utajiri, hekima, na ujuzi wa mipango na upendo wa Mungu, na wachochewe kumshukuru Mungu mwenyewe ambaye kupitia wema wake amewezesha kuchapishwa kwa kichapo hiki.”

  • Makasisi Wawili Waliothamini Vitabu vya Russell
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Aprili 15
    • “Ilionekana Kama Magamba Yameanguka Kutoka kwa Macho Yangu”

      Kasisi mwingine wa Wawaldo aliyethamini vichapo vya Russell alikuwa Giuseppe Banchetti. Giuseppe alifundishwa mafundisho ya Wawaldo na babake aliyeacha Ukatoliki. Mwaka wa 1894, Giuseppe akawa kasisi na akahudumia jumuiya kadhaa za Wawaldo huko Apulia na Abruzzi na katika visiwa vya Elba na Sicily.

      Mashahidi wa Yehova walichapisha kitabu cha Russell, Divine Plan of the Ages, katika Kiitalia mwaka wa 1905. Banchetti aliandika maoni yenye kusisimua kuhusu kitabu hicho. Maoni yake yalichapishwa katika jarida la Waprotestanti La Rivista Cristiana. Banchetti aliandika: ‘Kwa upande wetu, kitabu cha Russell ndiyo njia nyangavu na hakika zaidi ya kuongoza Mkristo yeyote kujifunza Maandiko Matakatifu kwa njia yenye kunufaisha na kuthawabisha. Punde tu baada ya kukisoma, ilionekana kana kwamba magamba yameanguka kutoka kwa macho yangu, na kwamba njia ya kumjua Mungu ilikuwa imenyooka zaidi na kuwa rahisi zaidi. Hata sikuona mambo ambayo hapo awali yalionekana kuwa yanapingana. Mafundisho ambayo hapo awali yalionekana kuwa magumu kueleweka yalionekana rahisi na yenye kukubalika kabisa. Mambo ambayo hayakueleweka hapo awali yakawa wazi zaidi. Nilielewa kwa urahisi mpango wenye kuvutia sana wa kuokoa ulimwengu kupitia Kristo hivi kwamba nilichochewa kusema maneno haya ya Mtume: Lo! kina cha utajiri wa Mungu na hekima na ujuzi!’—Waroma 11:33.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki