-
Historia Sahihi, Wala Si HadithiMnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
-
-
MFANO: Biblia inasema kwamba “Nebukadneza mfalme wa Babiloni . . . [aka]mpeleka Yehoyakini [Mfalme wa Yuda] uhamishoni Babiloni.” Baadaye, “Evil-merodaki mfalme wa Babiloni, katika mwaka wa kuwa kwake mfalme, akakiinua kichwa cha Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka katika nyumba ya kifungo.” Zaidi ya hayo, “[Yehoyakini] alipewa posho daima kutoka kwa mfalme, kila siku kama inavyostahili, siku zote za maisha yake.”—2 Wafalme 24:11, 15; 25:27-30.
MAMBO AMBAYO WATAALAMU WA VITU VYA KALE WAMEGUNDUA: Katika magofu ya Babiloni la kale, wataalamu wa vitu vya kale waligundua hati za usimamizi zilizokuwa na tarehe ya wakati wa utawala wa Nebukadneza wa Pili. Hati hizo zina orodha ya kiwango cha chakula ambacho wafungwa na watu wengine waliotegemea nyumba ya kifalme walipewa. Orodha hiyo inatia ndani “Yaukini [Yehoyakini],” ambaye alikuwa “mfalme wa nchi ya Yahud (Yuda),” pamoja na familia yake.
-
-
Historia Sahihi, Wala Si HadithiMnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 5]
Hati yA Babiloni inayomtaja Mfalme Yehoyakini wa Yuda
[Picha Hisani katika ukurasa wa 5]
© bpk, Berlin/Vorderasiatisches Museum, SMB/Olaf M. Tessmer/Art Resource, NY
-