-
Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako?Amkeni!—1997 | Juni 8
-
-
Hasira iliyodhibitiwa yaweza kuwa sawa. Mathalani, hasira ya Mungu iliwaka dhidi ya miji ya kale isiyo ya adili ya Sodoma na Gomora. (Mwanzo 19:24) Kwa nini? Kwa sababu wakazi wa miji hiyo walijihusisha na jeuri na mazoea ya ngono zilizopotoka, kama ilivyojulikana katika eneo lote. Mathalani, wajumbe wa kimalaika walipomtembelea Loti mwadilifu, kikundi cha wafanya-ghasia cha vijana pamoja na wazee kilijaribu kuwabaka kwa pamoja wageni wa Loti. Kwa halali Yehova Mungu alichukizwa na ukosefu wao mbaya sana wa adili.—Mwanzo 18:20; 19:4, 5, 9.
-
-
Kwa Nini Udhibiti Hasira Yako?Amkeni!—1997 | Juni 8
-
-
Hivyo, kuna tofauti kati ya Mungu na mwanadamu. Yehova aweza ‘kuiacha hasira yake’ na kwa haki afafanuliwa kuwa “si mwepesi wa hasira” kwa sababu upendo ndio sifa yake kuu, wala si hasira. Sikuzote hasira yake ni ya uadilifu, sikuzote ni halali, sikuzote imedhibitiwa. (Kutoka 34:6, NW; Isaya 48:9; 1 Yohana 4:8)
-