Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Imani ya Wazazi Yathawabishwa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
    • Ilikuwa ni wakati huo wa jaribio hilo ovu sana la kuangamiza jamii nzima-nzima kwamba Amramu na Yokebedi, wenzi waliooana Waebrania, walipozaa mtoto mchanga, mzuri mvulana. Ni rahisi kuwazia jinsi shangwe yao ilivyofunikwa na woga walipokumbuka agizo la Farao. Hata hivyo, Amramu na Yokebedi walipomwangalia mtoto wao mchanga mvulana, waliazimia kwa uthabiti kutomwacha, hata matokeo yaweje.—Kutoka 2:1, 2; 6:20.

      Kutenda kwa Imani

      Kwa miezi mitatu Amramu na Yokebedi walimficha mtoto wao mchanga. (Kutoka 2:2) Hata hivyo, hilo lilikuwa hatari, kwa kuwa Waebrania na Wamisri waliishi karibu-karibu. Yamkini yeyote aliyepatikana akijaribu kuhepa agizo la Farao angeadhibiwa kwa kuuawa—na huyo mtoto mchanga angeuawa pia. Hivyo basi, wazazi hao wenye kujitoa wangeweza kufanya nini ili mwanao na wao wenyewe waendelee kuwa hai?

      Yokebedi alikusanya machipukizi ya mafunjo. Mafunjo ni tete ngumu, sawa na mianzi, na yana mabua yenye pande tatu zenye unene upatao wa kidole. Yaweza kufika kimo cha meta sita. Wamisri walitumia mmea huo kutengeneza karatasi, mikeka, tanga, makubazi, na mashua nyepesi.

      Yokebedi alitengeneza kwa mafunjo kisanduku chenye kutoshea mtoto wake mchanga. Kisha akakipaka lami na bereu kukiunganisha na kukifanya kisivuje maji. Ndipo Yokebedi akamweka mtoto wake mchanga ndani ya hicho chombo na kukiweka katikati ya tete ukingoni mwa Mto Naili.—Kutoka 2:3.

  • Imani ya Wazazi Yathawabishwa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
    • Yokebedi alimlea mtoto wake hadi alipoachishwa kunyonya.c Hilo lilimpa fursa nyingi zenye thamani za kumfundisha juu ya Mungu wa kweli, Yehova. Kisha Yokebedi akamrudisha mtoto kwa binti Farao, aliyemwita huyo mvulana Musa, jina linalomaanisha ‘alitolewa majini.’—Kutoka 2:10.

      Somo Kwetu Sisi

      Amramu na Yokebedi walitumia kikamili fursa fupi waliyopata kumfundisha mwana wao kanuni za ibada safi. Wazazi leo wapaswa kufanya hivyohivyo. Kwa kweli, ni muhimu wafanye hivyo. Shetani Ibilisi “hutembea huku na huku kama simba anayenguruma, akitafuta sana kunyafua mtu fulani.” (1 Petro 5:8) Angependa vijana wenye thamani wawe wahasiriwa wake—wavulana na wasichana—walio na tazamio la kuwa watumishi wazuri wa Yehova. Umri wao mchanga haumfanyi Shetani awaonee huruma vijana! Kwa sababu hiyo, wazazi wenye hekima huzoeza watoto wao wachanga kumhofu Mungu wa kweli, Yehova.—Mithali 22:6; 2 Timotheo 3:14, 15.

      Kwenye Waebrania 11:23, ile jitihada ya Amramu na Yokebedi kumficha mtoto wao mchanga katika miezi mitatu ya kwanza ya maisha yake imerekodiwa kuwa tendo la imani. Wazazi hao wawili wenye kuhofu Mungu walionyesha itibari katika uwezo wa Yehova wa kuokoa kwa kukataa kumwacha pekee mtoto wao, na kwa ajili ya hilo walibarikiwa. Sisi pia twapaswa kuonyesha ushikamano kabisa kwa sheria na kanuni za Yehova, tukiwa na uhakika kwamba chochote ambacho Yehova huruhusu kitupate hatimaye kitatokeza hali-njema na furaha ya milele.—Waroma 8:28.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki