-
Ujumbe Mtamu na MchunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na sauti ambayo mimi nilisikia kutoka katika mbingu inanena tena na mimi na kusema: ‘Nenda, kachukue hati-kunjo iliyo katika mkono wa malaika ambaye anasimama juu ya bahari na juu ya dunia.’ Na mimi nikaenda kwa malaika na nikamwambia anipe mimi hati-kunjo ndogo. Na yeye akasema kwangu mimi: ‘Ichukue na uile yote, na itafanya tumbo lako kuwa chungu, lakini katika kinywa chako itakuwa tamu kama asali.’ Na mimi nikachukua hati-kunjo ndogo kutoka mkono wa malaika na mimi nikaila yote, na katika kinywa changu ilikuwa tamu kama asali; lakini wakati mimi nilipokuwa nimeila, tumbo langu lilifanywa kuwa chungu. Na wao husema kwangu mimi: ‘Wewe ni lazima utoe unabii tena kwa habari ya vikundi vya watu na mataifa na ndimi na wafalme wengi.’”—Ufunuo 10:8-11, NW.
16. (a) Nabii Ezekieli alikuwaje na ono kama la Yohana? (b) Ni kwa nini hati-kunjo ndogo ilikuwa na ladha tamu kwa Yohana, lakini kwa nini ikawa chungu kutulia tumboni?
16 Ono la Yohana ni kama lile la nabii Ezekieli wakati wa uhamisho katika bara la Babuloni. Yeye pia aliamriwa ale hati-kunjo iliyokuwa na ladha tamu katika kinywa chake. Lakini wakati ilipojaa tumbo lake, ilimfanya awe na daraka la kutabiri vitu vichungu kwa nyumba ya Israeli yenye kuasi. (Ezekieli 2:8–3:15) Hati-kunjo iliyofunguliwa ambayo Yesu Kristo aliyetukuzwa anampa Yohana hali kadhalika ni ujumbe wa kimungu. Yohana anapaswa kuhubiria “vikundi vya watu na mataifa na ndimi na wafalme wengi.” Kujilisha hati-kunjo hii ni kutamu kwake kwa sababu inatokana na chanzo cha kimungu. (Linga Zaburi 119:103; Yeremia 15:15, 16.) Lakini yeye anaiona kuwa chungu kutulia tumboni kwa sababu—kama ilivyokuwa kwa Ezekieli wakati uliopita—inatabiri mambo yasiyo matamu kwa binadamu waasi.—Zaburi 145:20.
-
-
Ujumbe Mtamu na MchunguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
20. Kula kwa Yohana hati-kunjo ndogo kulikuwa picha ya nini?
20 Kula kwa Yohana hati-kunjo yote kulitoa picha ya kwamba ndugu za Yesu walikubali mgawo huu. Ukawa sehemu yao kwa kadiri ya kwamba wao walikuwa wamehusianishwa na sehemu hii ya Neno la Mungu lililovuviwa, wakipata ulishaji kutokana nayo. Lakini walichopaswa kuhubiri kilikuwa na semi za hukumu za Yehova ambazo zilikuwa si tamu kwa wengi wa aina ya binadamu. Kweli kweli, kilitia ndani tauni zilizotabiriwa katika Ufunuo sura ya 8. Hata hivyo, ilikuwa tamu kwa Wakristo hawa wenye mioyo myeupe kujua hukumu hizo na kung’amua kwamba wao walikuwa wakitumiwa tena na Yehova katika kupiga mbiu yazo.—Zaburi 19:9, 10.
-