-
Mashahidi wa Yehova Wasonga Mbele Wakiwa na Usadikisho Imara!Mnara wa Mlinzi—2001 | Januari 15
-
-
“Mradi wetu mwaka huu ni kujenga Majumba ya Ufalme 240 zaidi,” akasema Robert Tracy, mratibu wa Halmashauri ya Ofisi ya Tawi. “Na bado,” akaongeza, “twahitaji mengine mengi.”
-
-
Mashahidi wa Yehova Wasonga Mbele Wakiwa na Usadikisho Imara!Mnara wa Mlinzi—2001 | Januari 15
-
-
Wakati huu, kuna uhitaji wa Majumba ya Ufalme elfu kadhaa katika eneo linalosimamiwa na ofisi ya tawi huko Afrika Kusini. Tayari majumba mengi sana yamejengwa. “Badala ya kukutania ndani ya banda au chini ya mti, kama walivyokuwa wakifanya hapo awali, ndugu zetu wanaweza kukutania mahali pafaapo, wakiwa na viti vifaavyo,” akasema John Kikot, mshiriki wa Halmashauri ya Ofisi ya Tawi. “Ingawa mengi ya Majumba hayo ya Ufalme hayakujengwa kwa gharama kubwa, kwa kawaida majengo hayo ndiyo yenye kuvutia zaidi katika maeneo yalikojengwa. Katika maeneo mengine, imeonwa kwamba baada ya kujenga Jumba la Ufalme, hudhurio la kutaniko huongezeka zaidi ya mara mbili mwaka unaofuata.”
-