-
Jifunze Kuhusu WabatakAmkeni!—2010 | Agosti
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 17]
ZIWA BARIDI LILILOTOKEZWA KWA MOTO
Ziwa Toba lina urefu wa kilomita 87 na upana wa kilomita 27, nalo ndilo ziwa kubwa zaidi ulimwenguni lililotokezwa na mlipuko wa volkano. Lina maji mengi sana baridi ambayo yanaweza kufunika nchi yote ya Uingereza kwa kina cha mita moja hivi. Likiwa limezungukwa na vilele vya milima ya volkano ambayo ni sehemu ya safu ya Milima ya Barisan, ziwa hilo maridadi hupendwa sana na wapiga-picha.
Ziwa hilo lilitokezwa na mlipuko mmoja au zaidi ya volkano, ambayo wanasayansi wanasema kwamba huenda ikawa ndiyo iliyokuwa milipuko yenye nguvu zaidi kuwahi kutokea katika historia. Baada ya muda, shimo kubwa sana lililotokea lilijaa maji na kutokeza Ziwa Toba. Milipuko kadhaa chini ya ziwa hilo ilitokeza Kisiwa maridadi cha Samosir, ambacho kimeenea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita 647 za mraba, ukubwa unaokaribia ule wa Jamhuri ya Singapore.
[Sanduku katika ukurasa wa 18]
PARADISO YENYE HALI NZURI YA HEWA
Ingawa Ziwa Toba liko kilomita 300 hivi kutoka kwenye ikweta, inashangaza kwamba eneo hilo lina baridi. Sababu ni kwamba ziwa hilo liko mita 900 juu ya usawa wa bahari. Mitende na misonobari hukua kwenye paradiso hiyo yenye joto la kadiri.
Ziwa hilo ndilo huwatenganisha wanyama fulani. Kwa mfano, orangutangu, sokwe wadogo wanaoitwa white-handed gibbon, na tumbili wanaiotwa Thomas’ leaf huishi upande wa kaskazini wa ziwa hilo, huku tapir, tarsier, na tumbili fulani walio na milia hupatikana upande wa kusini.
-
-
Jifunze Kuhusu WabatakAmkeni!—2010 | Agosti
-
-
[Ramani katika ukurasa wa 16]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Sumatra
Ziwa Toba
[Hisani]
Based on NASA/Visible Earth imagery
[Picha katika ukurasa wa 16, 17]
Ziwa Toba unapolitazama kutoka Mlima Pusuk Buhit
[Picha katika ukurasa wa 18]
Poromoko la maji la Sipisopiso, lililo katika ncha ya kaskazini ya Ziwa Toba, lenye urefu wa mita 110
-