Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Zile Nyota na Vile Vinara vya Taa

      5. Yesu anaelezaje “zile nyota saba” na “vile vinara vya taa saba”?

      5 Yohana amemwona Yesu akiwa katikati ya vinara vya taa saba vya dhahabu akiwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia. (Ufunuo 1:12, 13, 16) Sasa Yesu anaeleza hilo: “Kwa habari ya siri takatifu ya zile nyota saba ambazo wewe uliona juu ya mkono wangu wa kulia, na ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu: Zile nyota saba humaanisha malaika wa yale makundi saba, na vile vinara vya taa saba humaanisha makundi saba.”—Ufunuo 1:20, NW.

  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 9. (a) Vile vinara vya taa saba vinawakilisha nini, na ni kwa nini vinara vya taa ni mfano unaofaa kwa hao? (b) Ile njozi ingeelekea kumkumbusha mtume Yohana kitu gani?

      9 Vile vinara vya taa saba ni makundi saba ambayo kwayo Yohana anaelekeza kitabu cha Ufunuo: Efeso, Smirna, Pargamamu, Thiatira, Sardisi, Filadelfia, na Laodikia. Ni kwa nini makundi yanafananishwa na vinara vya taa? Ni kwa sababu Wakristo, wawe mmoja mmoja au kwa ujumla kama kundi, sharti ‘waache taa zao ziangaze mbele ya watu’ katika huu ulimwengu wenye kutiwa giza. (Mathayo 5:14-16) Kwa kuongezea, vinara vya taa vilikuwa miongoni mwa samani za hekalu la Solomoni. Kuyaita makundi vinara vya taa inaelekea kungemkumbusha Yohana kwamba, katika maana ya kielezi, kila kundi la kienyeji, la wapakwa-mafuta ni “hekalu la Mungu,” mahali pa kukaliwa na roho ya Mungu. (1 Wakorintho 3:16) Zaidi ya hilo, katika mpango wa kinachofananishwa na hekalu la Kiyahudi, washiriki wa kundi la wapakwa-mafuta wanatumikia wakiwa “ukuhani wa kifalme” katika mpango mkubwa wa hekalu la kiroho la Yehova, ambalo Yesu ndiye Kuhani Mkuu na ambamo Yehova anakaa kibinafsi katika Patakatifu Zaidi Sana pa kimbingu.—1 Petro 2:4, 5, 9; Waebrania 3:1; 6:20; 9:9-14, 24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki