-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
19. (a) Yale makundi saba yanafananisha nini leo? (b) Ni nani ambao wameshirikiana na Wakristo wapakwa-mafuta wakiwa hesabu kubwa-kubwa na kwa nini lile shauri la Yesu na hali anazoeleza Yesu huhusu wao pia? (c) Imetupasa sisi tuzioneje zile jumbe za Yesu kwa yale makundi saba ya karne ya kwanza?
19 Kwa sababu hii, maneno ya Yesu kwa yale makundi yamekuwa na utumizi wayo mkubwa tangu 1914. Katika mazingira haya, yale makundi saba yanafananisha makundi yote ya Wakristo wapakwa-mafuta katika kipindi cha hii siku ya Bwana.
-
-
Washa Upya Upendo wa Kwanza!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Hivi ndivyo vitu ambavyo yeye anasema ambaye hushika zile nyota saba katika mkono wake wa kulia, yeye ambaye hutembea katikati ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu.” (Ufunuo 2:1, NW) Kama ilivyo katika zile jumbe nyingine sita, hapa Yesu anavuta fikira kwenye jambo moja linaloonyesha cheo chake chenye mamlaka. Yeye anakumbusha wale waangalizi wa Efeso kwamba wazee wote wako chini ya uangalizi wake mwenyewe wenye himaya na kwamba yeye anakagua makundi yote. Kuteremka kuingia ndani ya nyakati zetu wenyewe, yeye ameendelea kutumia ukichwa huu wenye upendo, akiwalinda wazee na akichunga kwa fadhili wote wanaoshirikiana na kundi. Wakati kwa wakati, yeye hurekebisha mipango ya kundi ili kuwezesha nuru ing’ae kwa uangavu zaidi. Ndiyo, Yesu ndiye Mchungaji Mkuu juu ya kundi la Mungu.—Mathayo 11:28-30; 1 Petro 5:2-4.
-