Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuwasaidia Wachina Huko Mexico
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
    • Ili wahubiri wengi zaidi waweze kuwasaidia watu hao wanaozungumza Kichina, masomo ya miezi mitatu yalianzishwa ili kuwafundisha Mashahidi huko Mexico jinsi ya kuhubiri kwa njia rahisi katika Kichina cha Mandarin. Mashahidi 25 walipata masomo hayo. Masomo hayo yalipomalizika, ofisa mmoja wa jamii ya watu wanaozungumza Kichina cha Mandarin huko Mexico City alihudhuria sherehe ya kuhitimu, na hilo lilionyesha jinsi watu wanaozungumza Kichina walivyochochewa na masomo hayo. Taasisi moja ya Kichina katika eneo hilo iliwafadhili wanafunzi watatu ili waende katika nchi nyingine kupata masomo yatakayowawezesha kujua Kichina vizuri zaidi.

      Masomo hayo ya lugha yalitia ndani mazoezi. Baada ya kujifunza sentensi chache za msingi, wanafunzi walianza kuhubiri kwa Kichina katika eneo la biashara la Mexico City. Wanafunzi hao wenye bidii walianzisha mafunzo ya Biblia 21. Broshua Mungu Anataka Tufanye Nini? katika Kichina iliyo na maandishi yenye herufi za Kiroma, zinazoitwa Pinyin, ilisaidia sana.

      Mashahidi waliokuwa wameanza tu kujifunza Kichina walifanikiwaje kuongoza mafunzo ya Biblia? Mwanzoni, walisema tu, “Qing Du [Tafadhali soma]” na kuonyesha fungu, kisha swali. Mtu aliposoma fungu na kujibu katika Kichina, walisema, “Shei shei [Asante]” na, “Hen Hao [Vema sana].”

  • Kuwasaidia Wachina Huko Mexico
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 17]

      Darasa la Kichina huko Mexico City

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki