-
Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Wakati wa miezi iliyofuata, wakuu wa Nazi walikataa katakata mashtaka yaliyofanywa katika azimio hilo lililochapwa. Kwa hiyo, katika Juni 20, 1937, Mashahidi waliokuwa wangali huru waligawanya ujumbe mwingine, barua iliyoandikiwa wakuu katika magazeti ya umma ambayo ilifichua wazi mambo mengi kwa urefu juu ya mnyanyaso huo, hati hiyo ilitaja majina ya maofisa na tarehe na mahali pa mnyanyaso. Mshangao ulikuwa mkuu miongoni mwa Gestapo juu ya mfichuo huo na juu ya uwezo wa Mashahidi wa kufanya ugawanyaji kama huo.
-
-
Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 448]
Katika Ujerumani, Mashahidi wa Yehova walieneza sana hadharani barua hii iliyoandikiwa maofisa kupitia magazeti ya habari katika 1937, hata ingawa ibada yao ilikuwa chini ya marufuku ya serikali
-