Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutumia Kileo Vibaya—Kunaathiri Afya
    Amkeni!—2005 | Oktoba 8
    • Ugonjwa wa Ini na Kansa

      Ini hufanya kazi muhimu ya kuyeyusha chakula, kuzuia maambukizo, kudhibiti mzunguko wa damu, na kuondoa vitu vyenye sumu mwilini, kutia ndani kileo. Kutumia kileo kwa muda mrefu huharibu ini katika hatua tatu. Katika hatua ya kwanza, kuvunjwa-vunjwa kwa ethanoli hufanya mafuta yasimeng’enywe haraka, na hivyo kuyafanya yarundamane kwenye ini. Baada ya muda, ini huvimba au mtu hupatwa na mchochota wa ini. Ingawa kileo kinaweza kumfanya mtu apatwe na mchochota wa ini, inaonekana kwamba pia kinaweza kupunguza uwezo wa mwili wa kupigana na virusi vya mchochota wa ini aina ya B na C.a Uvimbe huo usipotibiwa, chembe hupasuka na kufa. Madhara hayo huongezeka kwani inaonekana kwamba kileo huchochea utendaji wa asili wa chembe kujiharibu.

      Hatua ya mwisho ni kunyauka kwa ini. Kadiri ini linavyoendelea kuvimba na chembe zake kuharibika, ndivyo kunavyokuwa na madhara yasiyoweza kurekebika. Mwishowe, ini huwa gumu badala ya kuwa laini kama sponji. Hatimaye, tishu zilizoathiriwa huzuia damu isizunguke kwa ukawaida na kufanya ini liache kufanya kazi na kusababisha kifo.

      Kileo huathiri ini pia katika njia nyingine isiyoonekana waziwazi, yaani, ini hushindwa kujikinga na athari za vitu vinavyosababisha kansa. Mbali na kuchochea ukuzi wa kansa ya ini, kileo huongeza sana hatari ya kupata kansa ya kinywa, koromeo, zoloto, na umio. Isitoshe, kileo hufanya tezi za mate zilizo mdomoni ziweze kupenywa kwa urahisi zaidi na kemikali zilizo katika tumbaku zinazoweza kusababisha kansa, na hivyo kuwahatarisha wavutaji sigara zaidi. Wanawake ambao hunywa kileo kila siku wanakabili hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kansa ya matiti. Kulingana na uchunguzi mmoja, hatari ya kupata kansa ya matiti ilikuwa kubwa kwa asilimia 69 kati ya watu wanaokunywa kileo kuliko wale wasiokunywa.

  • Kutumia Kileo Vibaya—Kunaathiri Afya
    Amkeni!—2005 | Oktoba 8
    • a Kulingana na uchunguzi mmoja uliofanywa nchini Ufaransa, hatari ya kunyauka kwa ini ni maradufu kati ya wagonjwa wenye virusi vya mchochota wa ini aina ya C ambao hunywa sana kuliko ilivyo kati ya wagonjwa wanaokunywa kwa kiasi. Inapendekezwa kwamba watu wenye ugonjwa huo wanywe kileo kidogo sana au wasinywe hata kidogo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki