Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Desemba 1
    • JEANNE LOUISE CALMENT alikufa Agosti 4, 1997 (4/8/1997), katika mji wao, kusini-mashariki mwa Ufaransa. Alikuwa na umri wa miaka 122!

      Leo, maendeleo katika sayansi, matibabu, na katika taaluma nyingine yanawasaidia watu leo kuishi miaka mingi. Hata hivyo, si watu wengi wanaoishi kwa miaka mia moja au zaidi. Labda hiyo ndio sababu nyakati nyingine umri wao mkubwa hutangazwa katika vyombo vya habari kama ilivyotokea katika kisa cha Bibi Calment.

  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Desemba 1
    • Kulingana na ripoti iliyochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Idadi ya Watu ya Max Planck nchini Ujerumani, wataalamu walikadiria umri wa Bibi Calment, aliyetajwa mwanzoni, baada ya kukusanya “taarifa sahili na zinazoweza kuthibitishwa” ambazo Calment mwenyewe alitoa. Taarifa hizo zilihusu wakati matukio fulani yaliyomhusu yeye mwenyewe au watu wake wa ukoo, yalipotokea. Kisha, yale aliyosema yakalinganishwa na rekodi za umma, rekodi za mthibitishaji wa hati, rekodi za kanisa, na pia makala za magazeti ya habari na sensa za watu. Jambo la kufurahisha ni kwamba, hata ingawa haikuwa rahisi kuthibitisha kila jambo, uthibitisho wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja ulifanya iwezekane kuthibitisha muda ambao Calment aliishi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki