-
Onyesha Upendo NyumbaniAmkeni!—2007 | Agosti
-
-
Watoto wanahitaji upendo na wanapoukosa, hawakui vizuri. Katika miaka ya 1950, M. F. Ashley Montagu, mtaalamu wa tabia na tamaduni za wanadamu aliandika hivi: “Mwanadamu anahitaji hasa upendo ili akue vizuri; upendo ndio chanzo cha afya nzuri hasa katika miaka sita ya kwanza.” Watafiti wa kisasa wanakubaliana na maneno ya Montagu aliposema kwamba “watoto huathiriwa sana wasipoonyeshwa upendo wa kutosha.”
-
-
Onyesha Upendo NyumbaniAmkeni!—2007 | Agosti
-
-
Waambie watoto wako kwamba unawapenda. Yehova Mungu aliwawekea wazazi kielelezo kizuri kwa kumwonyesha Mwana wake, Yesu, upendo waziwazi. (Mathayo 3:17; 17:5) Fleck, baba anayeishi Austria, anasema: “Nimegundua kwamba watoto ni kama maua fulani. Kama vile mimea hiyo midogo hugeuka kuelekea jua ili kupata mwangaza na joto, watoto huwategemea wazazi wao ili wapate upendo na kuhakikishiwa kwamba wao ni washiriki wa familia wenye thamani.”
-