Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Hutujali Sikuzote
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Septemba 1
    • Baada ya mimi kuwa mjane, mwana-mkwe wangu alijitwalia daraka la kunitunza mimi pamoja na mke na watoto wake watano. Kwa kuhuzunisha, alikufa Agosti 2000, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Binti yangu angepataje chakula na makao kwa ajili yetu? Kwa mara nyingine tena, niliona kwamba Yehova anatujali, naye kwa kweli ni “baba wa yatima na mwamuzi wa wajane.” (Zaburi 68:5) Kupitia watumishi wake duniani, Yehova alituandalia nyumba mpya nzuri. Jinsi gani? Ndugu na dada zetu kutanikoni walipoona shida yetu, walitujengea nyumba kwa majuma matano tu! Ndugu kutoka makutaniko mengine ambao ni mafundi wa matofali walikuja kutusaidia. Tulifurahi sana kwa sababu ya upendo na fadhili ambazo Mashahidi hao walituonyesha kwa kuwa walitujengea nyumba bora kuliko nyumba ambazo wengi wao wanaishi. Upendo huo ambao kutaniko lilionyesha ulikuwa ushahidi mzuri sana kwa jirani zetu. Ninapolala usiku, mimi huhisi kana kwamba niko katika Paradiso! Naam, nyumba yetu mpya nzuri imejengwa kwa matofali na saruji, lakini kama vile ambavyo wengi wamesema, ni nyumba ambayo kwa kweli ilijengwa kwa upendo.—Wagalatia 6:10.

  • Yehova Hutujali Sikuzote
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Septemba 1
    • [Picha katika ukurasa wa 28]

      Nyumba iliyojengwa kwa upendo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki