-
Ulimwengu Uliojaa MaajabuAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
Hata hivyo, nishati isiyoonekana si kitu pekee kisichoonekana ambacho kimegunduliwa katika siku za karibuni. Kitu kingine kiligunduliwa katika miaka ya 1980 wataalamu wa nyota walipochunguza vikundi kadhaa vya nyota. Vikundi hivyo vya nyota, na vilevile kikundi chetu, vilionekana vinazunguka kwa kasi sana hivi kwamba haviwezi kushikamana. Basi uthibitisho unaonyesha kwamba mata fulani inatoa nguvu za uvutano zinazofanya vishikamane. Lakini hiyo ni aina gani ya mata? Kwa sababu wanasayansi hawajui mata hiyo, waliiita mata nyeusi, kwa kuwa haifyonzi, haitoi, au kutokeza kiasi fulani cha mnururisho.c Kuna kiasi gani cha mata nyeusi? Makadirio yanaonyesha kwamba huenda ni asilimia 22 au zaidi ya ulimwengu.
Fikiria hili: Kulingana na makadirio ya sasa, mata ya kawaida inafanyiza asilimia 4 hivi ya ulimwengu. Inaonekana kwamba mata nyeusi na nishati isiyoonekana vinafanyiza sehemu iliyobaki.
-
-
Ulimwengu Uliojaa MaajabuAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
c Wazo la kwamba kuna mata nyeusi lilianzishwa katika miaka ya 1930 na likathibitishwa katika miaka ya 1980. Leo wataalamu wa nyota wanapima kiasi cha mata nyeusi katika vikundi vingi vya nyota kwa kuchunguza jinsi vikundi hivyo vinavyopinda nuru kutoka kwa vitu vilivyo mbali.
-
-
Ulimwengu Uliojaa MaajabuAmkeni!—2009 | Agosti
-
-
[Mchoro katika ukurasa wa 18]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Asilimia 74 nishati isiyoonekana
Asilimia 22 mata nyeusi
-