-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Oktoba 1
-
-
Dhabihu za wanyama zilikuwa sehemu muhimu ya sherehe katika mahekalu ya Wagiriki na Waroma, lakini nyama yote iliyotolewa dhabihu haikuliwa wakati wa sherehe. Hivyo, nyama iliyobaki kwenye mahekalu hayo ya kipagani iliuzwa sokoni. Kitabu kimoja (Idol Meat in Corinth) kinasema: “Viongozi wa madhehebu . . . nyakati nyingine wanaitwa wapishi na/au wachinjaji. Nyama waliyopewa kama malipo kwa kuchinja mnyama aliyetolewa dhabihu, waliiuza sokoni.”
Kwa hiyo, si nyama zote zilizouzwa sokoni ambazo zilikuwa mabaki ya nyama zilizotumiwa katika sherehe za kidini. Kwa kuwa, viunzi vizima vya mifupa ya kondoo vilichimbuliwa katika eneo la soko la nyama (Kilatini, macellum) la Pompeii. Msomi Henry J. Cadbury anasema jambo hilo linadokeza kwamba “huenda nyama zilizouzwa ni za wanyama hai au wanyama waliochinjwa kwenye macellum na pia nyama za wanyama waliochinjwa au kutolewa dhabihu hekaluni.”
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Oktoba 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 12]
Sahani ya udongo iliyo na picha ya watu wakitoa dhabihu ya wanyama katika karne ya sita K.W.K.
[Hisani]
Musée du Louvre, Paris
-