Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 3/8 uku. 31
  • Mauzo ya Kidini ya Kutoa Msaada

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mauzo ya Kidini ya Kutoa Msaada
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • “Sanamu kwa Ajili ya Ibilisi Mwenyewe”
    Amkeni!—2002
  • Hawakuinamia Sanamu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Sababu Inayofanya Miujiza Peke Yayo Isijenge Imani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Je, Kweli Yesu Alikuwa na Imani Katika Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 3/8 uku. 31

Mauzo ya Kidini ya Kutoa Msaada

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Italia

ILIKUWA Februari 1995 kwamba ripoti zilianza kuenea kuhusu kile kilichofikiriwa kuwa muujiza wa siku ya kisasa: Sanamuumbo ya Madonna katika Civitavecchia kwa kuwazia ilionwa ikilia machozi ya damu. Tangu wakati huo, Wakatoliki kutoka sehemu zote za ulimwengu wameenda hija ili kujionea sanamuumbo hiyo.

Na bado kulingana na gazeti la habari La Repubblica, Wakatoliki wengi wanaudhiwa na “hali ya mauzo ya msaada” inayozingira eneo la hilo la watalii. Hata wanatheolojia kadhaa wana wasiwasi kuhusu matungamo ya watu yanayoenda kwa makundi kuipatia sanamuumbo hiyo heshima inayopita kiasi. Kwa kielelezo, Luigi Pizzolato, mwalimu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Milan, anakosoa kanisa kwa kuridhika na imani “inayoamshwa kihisia-moyo.” Aonelea kwamba matunda yanayotokezwa na unaosemekana kuwa muujiza “yameharibu ubora na ushirikina.” Mwanatheolojia mwingine, Carlo Molari, atukumbusha kwamba, “katika Agano Jipya, mtu fulani aliyeitwa Simon Magus atumia nguvu zisizo za kawaida kwa ajili ya faida yake—kujipatia pesa, tungesema hivyo leo.”—Matendo 8:9-24.

Yesu aliwaonya wanafunzi wake wajihadhari na wale ambao wangefanya ishara “zilizo kubwa na maajabu.” (Mathayo 24:3, 24) Hata wakati ishara kama hizo zionekanapo kuwa halisi, imani ya Mkristo haiwezi kutegemezwa juu ya miujiza ya kudhaniwa. (Waebrania 11:1, 6) Badala ya hivyo, ni kwa kujipatia ujuzi sahihi wa Neno la Mungu na kutumia shauri lake ndipo imani thabiti inapoweza kupatikana. (Yohana 17:3; Waroma 10:10, 17; 2 Timotheo 3:16) Je, ungependa kuwa na imani ya aina hiyo? Kwa nini usiache Mashahidi wa Yehova wakusaidie wanapokutembelea wakati ujao?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

AGF/La Verde

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki