-
Mwaka wa Kipekee wa EinsteinAmkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
Sababu Inayofanya Chavuo Zicheze Dansi
Mnamo 1905, Einstein alianza kuchunguza atomu na molekyuli. Alifafanua jinsi vitu hivyo huathiri chembe za chavuo zilizo juu ya maji. Mnamo 1827, mwanabiolojia anayeitwa Robert Brown aliangalia kwa kutumia darubini na kutambua kwamba chembe za chavuo zinapokuwa ndani ya maji hucheza-cheza. Aliita dansi hiyo ya chavuo msogeo wa Brown, lakini hakuweza kueleza sababu iliyofanya zicheze-cheze.
Katika hati yake ya Mei 1905, Einstein alieleza jinsi molekyuli za maji zinazotikisika zilivyosababisha msogeo huo wa Brown. Alikadiria ukubwa wa molekyuli za maji na pia akaeleza kimbele jinsi atomu za molekyuli hizo zilivyo. Wanasayansi wengine walitumia maelezo yake kuwa msingi wa kufanya utafiti, na hivyo kuondoa shaka kuhusu kuwepo kwa atomu hizo. Fizikia ya kisasa hutegemea nadharia ya kwamba mata imefanyizwa kwa atomu.
-
-
Mwaka wa Kipekee wa EinsteinAmkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 21]
(See publication)
Dansi ya msogeo wa Brown ilisaidia kuthibitisha kuwepo kwa atomu
-