Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Toledo—Mchanganyiko wa Utamaduni wa Enzi za Kati
    Amkeni!—2007 | Juni
    • Minara mingi ya ukumbusho yenye kupendeza huko Toledo ni ya kipindi cha enzi za kati. Watawala Wakatoliki walifanya Toledo kuwa jiji lao kuu, Wayahudi walitengeneza vyombo vya sanaa na kufanya biashara, nao mafundi Waislamu walitumia ustadi wao kuchora ramani za ujenzi.

  • Toledo—Mchanganyiko wa Utamaduni wa Enzi za Kati
    Amkeni!—2007 | Juni
    • Minara ya Ukumbusho

      Leo sehemu ya katikati ya jiji la Toledo ina minara ya ukumbusho zaidi ya mia moja. Kwa sababu hiyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni lilitangaza Toledo kuwa Jiji Linalostahili Kuhifadhiwa Ulimwenguni. Majengo mawili yenye kupendeza yaliyojengwa katika enzi za kati ni madaraja yaliyo juu ya Mto Tagus. Daraja moja linawezesha watu wanaotoka mashariki wafike jijini na lile la pili linawawezesha watu wa magharibi wafike jijini. Na ni wageni wachache tu ambao hukosa kuona lango kubwa la Puerta Nueva de Bisagra lililo nje ya jiji la kale lililozingirwa kwa kuta.

      Mtu akiwa mbali ataona minara miwili mirefu ya ukumbusho. Upande wa mashariki kuna ngome kubwa ya mraba inayoitwa Alcázar. Kwa karne nyingi imetumika kama makao ya gavana Waroma, makao ya wafalme Wavisigothi, ngome ya Waarabu, na makao ya wafalme Wahispania. Sasa Jumba la Ukumbusho la Jeshi na maktaba kubwa inapatikana huko. Lakini kwa kuwa Toledo hasa ni jiji la kidini, kuna kanisa kubwa la Kigothi katikati ya jiji hilo.—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 17.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki