-
“Mayday! Mayday! Mayday!” Mwito Ambao Huokoa UhaiAmkeni!—2010 | Oktoba
-
-
Njia Nzuri Zaidi za Kuomba Msaada
Katika miaka ya 1840 kulikuwa na maendeleo makubwa katika teknolojia ya mawasiliano. Samuel Morse alivumbua njia ya kuwasiliana ambayo watu wangetumia telegrafu kutuma ujumbe kupitia waya iliyounganishwa kwenye kifaa cha kurushia habari. Kifaa hicho kilipobonyezwa, mtu aliye upande ule mwingine angeweza kusikia mlio fulani uliotokezwa na umeme. Morse alihakikisha kwamba kila herufi na nambari inawakilishwa na sauti, nukta, au kistari kifupi au kirefu.
Ili kuwasiliana kwa kutumia mfumo wa alama za siri wa Morse baharini, mabaharia walitumia miale ya nuru badala ya sauti zilizotumwa kwa telegrafu. Ikiwa mtu angeangaza mwale kwa muda mfupi, mwale huo ungewakilisha nukta, na ikiwa angemulika kwa muda mrefu zaidi mwale huo ungewakilisha kistari. Baada ya muda, watu walianza kutuma mwito mfupi wa kuomba msaada kwa kutumia nukta tatu, vistari vitatu, kisha nukta tatu zaidi, kumaanisha herufi SOS.b
Kwa kupendeza, bado watu waliendelea kubuni njia za kuomba msaada. Mnamo 1901, Guglielmo Marconi alituma ujumbe wa kwanza kwa kutumia mawimbi ya redio akiwa kwenye Bahari ya Atlantiki. Sasa ujumbe wa SOS ungetumwa kupitia mawimbi ya redio badala ya miale ya mwanga.
-
-
“Mayday! Mayday! Mayday!” Mwito Ambao Huokoa UhaiAmkeni!—2010 | Oktoba
-
-
b Herufi SOS zilichaguliwa kwa sababu zingetumwa kwa urahisi na kueleweka. Hazikuwa na maana hususa.
-
-
“Mayday! Mayday! Mayday!” Mwito Ambao Huokoa UhaiAmkeni!—2010 | Oktoba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 28]
Ili kuwasiliana kwa kutumia mfumo wa alama za siri wa Morse baharini, mabaharia walitumia miale ya nuru badala ya sauti zilizotumwa kwa telegrafu
[Hisani]
© Science and Society/SuperStock
-