-
Waandishi wa Zamani na Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
Waandishi Katika Israeli la Kale
Musa alilelewa katika nyumba ya Farao. (Kutoka 2:10; Matendo 7:21, 22) Kulingana na mtaalamu mmoja wa mambo ya kale ya Misri, huenda elimu ya Musa ilitia ndani kujifunza kusoma na kuandika maandishi ya Kimisri na angalau ustadi fulani-fulani wa uandishi. Katika kitabu chake (Israel in Egypt), Profesa James K. Hoffmeier anasema: “Kuna msingi wa kuamini wazo la kibiblia kwamba Musa alikuwa na uwezo wa kuandika matukio, kukusanya habari kuhusu safari, na kufanya kazi nyinginezo za uandishi.”b
-
-
Waandishi wa Zamani na Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
b Mambo ya kisheria ambayo Musa aliandika yanapatikana katika Kutoka 24:4, 7; 34:27, 28; na Kumbukumbu la Torati 31:24-26. Wimbo alioandika unapatikana katika Kumbukumbu la Torati 31:22, na habari alizokusanya kuhusu safari ya nyikani zimo katika Hesabu 33:2.
-