-
“Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote”Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
-
-
Hata hivyo, kuwapo kwa Mungu katika nyumba yake ya kidunia kuliwakilishwa na wingu katika chumba cha ndani zaidi cha Patakatifu Zaidi Sana. (Mambo ya Walawi 16:2) Kwa wazi, wingu hilo liling’aa kwa wangavu, likiandaa nuru katika Patakatifu Zaidi Sana. Lilikuwa juu ya sanduku takatifu lililoitwa “sanduku la ushuhuda,” lililokuwa na mabamba ya mawe yaliyonakshiwa baadhi ya amri ambazo Mungu aliwapa Waisraeli.
-
-
“Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote”Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
-
-
Wingu la nuru la kimuujiza lilikuwa juu ya kifuniko na kati ya makerubi. (Kutoka 25:22) Hilo ilionyesha wazo la Mungu Mweza Yote akiwa ametawazwa juu ya gari la kimbingu linalotegemezwa na makerubi walio hai. (1 Mambo ya Nyakati 28:18) Hiyo ndiyo sababu Mfalme Hezekia alisali hivi: “Ee BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi.”—Isaya 37:16.
-