-
Jinsi Hali ya Hewa Inavyoweza Kubadili HistoriaAmkeni!—2011 | Juni
-
-
Washindwa kwa Mvua
Tukio lingine lililobadili ulimwengu ambalo liliathiriwa sana na hali ya hewa ni Pigano la Waterloo la mwaka wa 1815. Historia inaonyesha kwamba katika vita hivyo vilivyopiganwa huko Waterloo, kilomita 21 kusini mwa Brussels, Ubelgiji, zaidi ya wanaume 70,000 waliuawa au kujeruhiwa kwa muda wa saa chache tu. Dyuki Mwingereza wa Wellington alichagua uwanja huo wa pigano na akachagua sehemu iliyokuwa imeinuka. Ingawa majeshi ya Ufaransa yaliyoongozwa na Napoleon yalikuwa mengi kuliko yale ya Wellington, Napoleon alihitaji kushinda maadui wake kabla ya giza kuingia, kwa sababu Wellington angepata askari zaidi wa kumsaidia kutoka kwa jeshi la Prussia usiku huo. Hata hivyo, kwa mara nyingine tena, hali ya hewa iliathiri sana mipango yake.
Mvua kubwa sana ilinyesha usiku uliotangulia vita hivyo. Wanajeshi wengi walikumbuka usiku huo kuwa usiku mgumu zaidi maishani mwao. Hata ingawa wengine wao walifaulu kusimamisha mahema madogo, mwanajeshi mmoja alisema kwamba vitanda vilivyokuwa ndani ya mahema hayo vilikuwa vimelowa kana kwamba vilikuwa ndani ya ziwa. Ardhi ililowa maji na kuwa kama kinamasi. Ili afaulu kushinda jeshi la Wellington, Napoleon alitaka kuanza mashambulizi yake alfajiri. Hata hivyo, hakufaulu kushambulia hadi baada ya saa kadhaa.
Sababu kuu iliyofanya achelewe kufanya mashambulizi hayo ni kwa sababu ardhi ilikuwa imelowa sana, ilihitajika ikauke kwa kiasi fulani ili vita vianze. Pia, matope yalizuia uwezo wa mizinga ambayo Napoleon alipendelea zaidi kutumia. Kwanza, ilikuwa vigumu kwao kusogeza vifaa hivyo kwenye matope na hilo likapunguza uwezo wao wa kurusha mizinga. Pili, matufe ya mizinga hiyo yalihitajika kugonga ardhi kisha yawalipukie wanajeshi wa Wellington kwa kadiri kubwa zaidi. Hata hivyo, yote hayo hayakuwezekana kwa sababu ardhi ilijaa matope, na hivyo mizinga haikuweza kulipuka kama ilivyokusudiwa. Hilo lilichangia sana kufanya Napoleon na majeshi yake washindwe. Hivyo, kwa sababu ya hali mbaya sana ya hewa, majeshi ya Napoleon yalishindwa, na akapelekwa uhamishoni.
-
-
Jinsi Hali ya Hewa Inavyoweza Kubadili HistoriaAmkeni!—2011 | Juni
-
-
[Picha katika ukurasa wa 25]
Pigano la Waterloo
[Hisani]
© Bettmann/CORBIS
-