Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika Mei 1924 Chama cha Nazi kilishikilia viti 32 katika Bunge la Ujeremani. Kufikia Mei 1928 vilikuwa vimepungua vikawa viti 12. Lakini, ule Mshuko Mkubwa wa Thamani ya Pesa ukagharikisha ulimwengu katika 1930; kufuata huo, Wanazi walipata nafuu yenye kutokeza, wakijipatia viti 230 kati ya 608 katika machaguzi ya Ujeremani ya Julai 1932. Hivyo, wakawa chama kikubwa zaidi ya vyote katika Bunge. Upesi baadaye, Franz von Papen, Mheshimiwa Kipapa, aliyekuwa Chansela hapo kwanza, akaja kusaidia Wanazi. Kulingana na wanahistoria, von Papen alikuwa na njozi ya Milki Takatifu ya Kiroma mpya. Muda wake mwenyewe mfupi wa kuwa Chansela ulikuwa umekuwa usiofanikiwa, hivyo sasa yeye alitumainia kujipatia mamlaka kupitia Wanazi. Kufikia Januari 1933, yeye alikuwa amepata uungaji-mkono kwa ajili ya Hitla kutoka kwa wenye viwanda, na kwa njama za hila yeye alihakikisha kwamba Hitla amekuwa Chansela wa Ujeremani katika Januari 30, 1933. Yeye mwenyewe alifanywa makamu wa Chansela na yeye alitumiwa na Hitla apate uungaji-mkono wa sehemu za Kikatoliki za Ujeremani. Kwa muda wa miezi miwili ya kujipatia mamlaka, Hitla alivunja bunge, akapeleka maelfu ya viongozi wapinzani kwenye kambi za mateso, na akaanza kampeni iliyo wazi ya kuwaonea Wayahudi.

      7 Katika Julai 20, 1933, upendezi wa Vatikani katika mamlaka iliyokuwa ikiinuka ya Unazi ulionyeshwa wakati Kardinali Pacelli (ambaye baadaye akawa Papa Pius 12) alipotia sahihi itifaki katika Roma kati ya Vatikani na Ujeremani ya Nazi. Von Papen alitia sahihi hati hiyo akiwa mwakilishi wa Hitla, na huko huko Pacelli akampa von Papen medali ya juu ya kipapa ya Msalaba Mtukufu wa Daraja la Pius.b Katika kitabu chake Satan in Top Hat, Tibor Koeves huandika juu ya hili, akitaarifu: “Itifaki ilikuwa ushindi mkubwa kwa ajili ya Hitla. Ilimpa uungaji-mkono wa kwanza wa kiadili aliokuwa amepokea kutoka ulimwengu wa nje, na huo kutoka chimbuko lililokwezwa zaidi sana.” Itifaki hiyo ilitaka Vatikani iondoe uungaji-mkono wayo kutoka kwa Chama cha Kati cha Kikatoliki, na hivyo kuidhinisha “serikali jumla” ya Hitla ya chama kimoja.c Zaidi, sehemu ya 14 yayo ilisema: “Uwekwaji rasmi wa maaskofu wakuu, maaskofu, na wengine kama hao utatolewa baada tu ya gavana, aliyewekwa na Serikali, kuhakikisha kabisa kwamba hakuna shaka lolote kwa habari ya mafikirio ya ujumla ya kisiasa.” Kufikia mwisho wa 1933 (uliotangazwa na Papa Pius 11 kuwa “Mwaka Mtakatifu”), uungaji-mkono wa Vatikani ulikuwa umekuwa umechangia sana jitihada kubwa ya Hitla kwa ajili ya utawala wa ulimwengu.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • b Kitabu cha historia cha William L. Shirer The Rise and Fall of the Third Reich hutaarifu kwamba von Papen alikuwa “mwenye daraka zaidi ya mwingine yeyote katika Ujeremani la Hitla kupata mamlaka.” Katika Januari 1933 aliyekuwa chansela wa Ujeremani von Schleicher alikuwa amesema hivi juu ya von Papen: “Yeye alithibitika kuwa aina ya haini ambaye kando yake Yudasi Iskariote ni mtakatifu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki