Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wa Kifumbo, na Bado ni Maridadi Mno
    Amkeni!—1996 | Januari 22
    • Kadiri Orioni anavyochipua mwendo kuelekea mbele, uta mkononi, yuaonekana kukabili kilimia cha Ng’ombe, yule fahali. Darubiniupeo ndogo itafunua, karibu na ncha ya pembe ya kusini ya fahali, kizio chenye nuru iliyofifia. Hicho chaitwa Kaa Nebula, na katika darubiniupeo kubwa, hicho chaonekana kama mlipuko unaoendelea, kama inavyoonyeshwa kwenye ukurasa 9. Ikiwa Orioni Nebula ni mahali pa kuzalia nyota, basi Kaa Nebula iliyo karibu tu huenda ikawa ziara la nyota yenye kupatwa na kifo kutokana na jeuri isiyowazika.

      Huo msiba wa kimbingu huenda ulipata kurekodiwa na waastronomia Wachina ambao walifafanua “Nyota Ngeni” katika Ng’ombe ambayo ilitokea kwa ghafula mnamo Julai 4, 1054, nayo ikang’aa kwa wangavu sana hivi kwamba ilionekana wakati wa mchana kwa siku 23. “Kwa majuma kadhaa,” akaonelea Robert Burnham, “hiyo nyota iliangaza kwa nuru ya jua zipatazo milioni 400.” Wanasayansi huita ujiuaji kimakusudi wa nyota ulio dhahiri kama huo supanova. Hata sasa, karibu miaka elfu moja baada ya kuonekana huko, vilipukaji kutoka kwa mlipuko huo vyazangaa angani kwa mwendo ukadiriwao kuwa kilometa milioni 80 kwa siku.

      Darubiniupeo ya Angani ya Hubble imekuwa ikichunguza nyanja hii pia, ikipekua ndani ya kitovu cha nebula na kuvumbua “mambo ya kindani katika Kaa ambayo waastronomia hawakutazamia kamwe,” kulingana na gazeti Astronomy. Mwastronomia Paul Scowen asema hayo mavumbuzi “lazima yatawafanya waastronomia wa kinadharia wafikirie sana kwa miaka mingi ijayo.”

      Waastronomia, kama vile Robert Kirshner wa Harvard, waamini kwamba kuelewa masalio ya supanova kama vile Kaa Nebula ni muhimu kwa sababu yaweza kutumiwa kupima umbali wa magalaksi mengineyo, ambayo sasa ni nyanja ya kufanyiwa utafiti sana. Kama tulivyoona, kutokubaliana juu ya umbali hadi magalaksi mengineyo hivi majuzi kumewasha mijadala mikali juu ya nadharia ya mshindo mkubwa kuhusu uumbaji wa ulimwengu wote mzima.

  • Wa Kifumbo, na Bado ni Maridadi Mno
    Amkeni!—1996 | Januari 22
    • Katika kitovu cha Kaa Nebula mna mojapo kitu cha ajabu kupita zote katika ulimwengu wote mzima unaojulikana. Kulingana na wanasayansi, kijizoga cha nyota iliyokufa, kikiwa kimebanwa ndani ya uzito usioaminika, huvurura katika kaburi lacho mara 30 kwa sekunde, kikitoa kasimawimbi za redio ambazo mara ya kwanza zilinaswa duniani katika 1968. Hicho huitwa pulsa, hufafanuliwa kuwa salio la supanova lenye kuvurura lililobanwa hivi kwamba elektroni na protoni katika atomu za nyota ya awali zimebanwa pamoja ili kutokeza nutroni. Wanasayansi husema kwamba wakati mmoja ilikuwa kiini kikubwa cha nyota kubwa mno kama ile ya Betelgeuse au Rigel katika Orioni. Hiyo nyota ilipolipuka na tabaka za nje kulipuliwa angani, ni kiini tu kilichobonyea ndicho tu kilibaki, kikiwa masao mangavu meupe, mioto yacho ya kinyukilia ilizima kitambo sana.

  • Wa Kifumbo, na Bado ni Maridadi Mno
    Amkeni!—1996 | Januari 22
    • Kaa Nebula katika Ng’ombe—ziara la nyota changa?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki