Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watu Waliounga Mkono Ibada ya Kweli Zamani za Kale na Leo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
    • Nehemia aliwagawia watu wa familia mbalimbali sehemu ya kazi hiyo kubwa ya kujenga upya ukuta, nao wakaifanya bega kwa bega.a Zaidi ya vikundi 40 tofauti vilipewa kazi ya kujenga upya “sehemu” mbalimbali za ukuta. Matokeo yakawa nini? Kazi hiyo ambayo ilionekana kuwa kubwa mno iliweza kukamilishwa kwa sababu wafanyakazi wengi sana, kutia ndani wazazi pamoja na watoto, walijitolea kutumia wakati na nguvu zao. (Nehemia 3:11, 12, 19, 20) Baada ya kujenga kwa bidii kwa muda wa miezi miwili, walimaliza kujenga upya ukuta wote! Nehemia aliandika kwamba hata wale waliokuwa wamepinga kazi ya kujenga upya ukuta walilazimika kutambua kwamba ‘kazi hiyo ilitendwa na Mungu wetu.’—Nehemia 6:15, 16.

  • Watu Waliounga Mkono Ibada ya Kweli Zamani za Kale na Leo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
    • a Andiko la Nehemia 3:5 linasema kwamba baadhi ya Wayahudi mashuhuri, “wakuu,” walikataa kusaidia kufanya kazi hiyo, lakini wengine wote waliiunga mkono. Watu wa malezi mbalimbali kama vile makuhani, mafundi wa dhahabu, mafundi wa manukato, wakuu, na wafanya-biashara, waliunga mkono mradi huo.—Mistari ya 1, 8, 9, 32.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki