Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mashua ya Galilaya—Hazina ya Nyakati za Biblia
    Amkeni!—2006 | Agosti
    • Kuna wavuvi, baadhi yao wakiwa katika mashua ndogo huku wengine wakitembea katika maji yasiyo na kina kirefu na kutupa nyavu zao. Kwa ustadi, wanatumia mkono mmoja tu kuvuta nyavu zao za mviringo ambazo zimefungiliwa vitu vizito kandokando. Nyavu hizo zina kipenyo cha kati ya meta 6 na 8. Nyavu hizo hujitandaza juu ya uso wa maji, kisha zinazama na kunasa samaki. Mvuvi hukusanya samaki kwa kukokota wavu hadi ufuoni au kwa kupiga mbizi na kubeba wavu pamoja na samaki. Biblia inasema kwamba Simoni na Andrea ‘walitupa’ nyavu zao. Huenda walifanya hivyo kwa njia kama ile iliyotajwa hapa.—Marko 1:16.

      Huenda ukaona wavuvi kadhaa wakizungumza kwa msisimko huku wakitayarisha wavu wa kukokotwa. Wavu huo unaweza kuwa na urefu wa meta 300, na kimo cha meta 8 kwenye sehemu ya katikati, ukiwa na kamba za kuvuta kwenye miisho yake. Wavuvi huchagua mahali watakapovua, kisha baadhi yao huenda ufuoni wakiwa wameshikilia kamba moja ya kukokota wavu huo. Mashua huingia majini na kusonga mbele kwa njia iliyonyooka, huku ikivuta wavu huo na kuunyoosha kabisa. Kisha mashua hiyo hugeuka na kuvuta wavu huo polepole na kufanyiza nusu duara kuelekea ufuoni. Wavuvi waliosalia hushuka nchi kavu wakiwa wameshika upande wa pili wa kamba ya kuvutia. Vikundi hivyo viwili vya wavuvi vinapokaribiana, wao huvuta samaki hadi ufuoni.—Mathayo 13:47, 48.

  • Mashua ya Galilaya—Hazina ya Nyakati za Biblia
    Amkeni!—2006 | Agosti
    • Giza linapoingia kimya hutanda kwenye ziwa hilo. Kwa ghafula, kimya hicho hukatizwa kwa makelele ya wavuvi wanaopigapiga miguu yao kwenye mashua na kupiga maji kwa makasia ili kutokeza kelele nyingi ajabu. Kwa nini? Wameshusha nyavu majini katika njia ambayo samaki, wakiwa wameogopeshwa na kelele hizo, huelekea moja kwa moja mtegoni. Wavu huo uliosimama wima, usioweza kuonekana gizani, umeundwa kwa njia ya kwamba samaki hunaswa kwa urahisi. Nyavu hizo hushushwa mara nyingi usiku wote. Asubuhi nyavu hizo husafishwa na kuanikwa. Huenda ukajiuliza, ‘Je, nyavu kama hizo ndizo zilitumika kuvua samaki kimuujiza kama inavyofafanuliwa kwenye Luka 5:1-7?’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki