Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu Mwenyewe
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kutoa Biblia Katika Namna Nyingi

      Kutumiwa kwa kompyuta katika shughuli za Watch Tower Society, kuanzia 1977, kumesaidia katika kutokezwa kwa Biblia, kama vile ambavyo kumesaidia katika njia nyinginezo za shughuli za uchapaji. Imesaidia watafsiri waweze kuwa na upatani zaidi katika kazi yao; pia imefanya iwe rahisi zaidi kuchapa Biblia katika namna mbalimbali.

      Baada ya maandiko yote ya Biblia kutiwa ndani ya kompyuta, haikuwa vigumu kutumia mashine ya kupanga chapa kwa kupiga picha kielektroni ili kuchapa maandiko yakiwa katika unamnanamna wa ukubwa na sura. Kwanza, katika 1981, kulitokezwa chapa ya ukubwa wa kawaida katika Kiingereza yenye konkodansi na mambo mengine ya nyongeza yenye kusaidia. Hiyo ndiyo iliyokuwa chapa ya kwanza kuchapwa na Watch Tower Society kwenye matbaa ya ofseti ya web. Baada ya masahihisho kuingizwa katika maandishi yaliyohifadhiwa ndani ya kompyuta, chapa yenye maandishi makubwa ya Kiingereza ilitolewa katika 1984; hiyo ilitia ndani sehemu nyingi muhimu kwa ajili ya utafiti. Chapa ya ukubwa wa kawaida ya Biblia ya Kiingereza iyo hiyo iliyosahihishwa ilitolewa pia mwaka huo; marejezo-vitomeo na konkodansi ilitiwa ndani, lakini si vielezi-chini; na nyongeza yayo ilibuniwa ifae huduma ya shambani badala ya funzo la kina kirefu zaidi. Kisha, kwa manufaa ya wale waliotaka chapa ndogo sana ya mfukoni, hiyo ilitangazwa katika Kiingereza katika 1987. Chapa hizo zote zilitangazwa upesi katika lugha nyinginezo pia.

      Kwa kuongezea, uangalifu ulitolewa ili kusaidia wale wenye mahitaji ya pekee. Ili kusaidia wale ambao wangeweza kuona lakini ambao walihitaji maandishi makubwa sana, New World Translation iliyo kamili ya lugha ya Kiingereza katika mabuku manne makubwa ilitangazwa katika 1985. Upesi chapa iyo hiyo ilichapwa katika Kijerumani, Kifaransa, Kihispania, na Kijapani. Kabla ya hapo, katika 1983, New World Translation of the Christian Greek Scriptures, katika mabuku manne, ilikuwa imetolewa katika Braille (chapa ya vipofu) ya Kiingereza cha gredi ya pili. Katika muda wa miaka mingine mitano, New World Translation iliyo kamili ilikuwa imetokezwa katika Braille ya Kiingereza katika mabuku 18.

      Je, watu fulani wangesaidiwa ikiwa wangeweza kusikiliza rekodi ya Biblia? Bila shaka. Kwa hiyo Watch Tower Society ilianza kutokeza hiyo pia. Kaseti ya kwanza iliyorekodiwa ilikuwa The Good News According to John, katika Kiingereza, iliyotolewa katika 1978. Baadaye New World Translation yote katika Kiingereza ilifanywa ipatikane katika kaseti 75. Ile iliyoanza ikiwa kazi ndogo upesi ilikua ikawa mradi mkubwa. Upesi, ilipatikana katika lugha nyinginezo. Kufikia 1992 New World Translation, ikiwa yote au kwa sehemu, ilipatikana katika kaseti katika lugha 14.

  • Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu Mwenyewe
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 614]

      “New World Translation” katika chapa kubwa sana

      . . . katika Braille

      . . . katika kaseti

      . . . katika disketi za kompyuta

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki