-
Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu MwenyeweMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Mifano fulani inaonyesha matokeo ya tafsiri hii. Katika Ufaransa, kwa karne nyingi Kanisa Katoliki lilikuwa limewakataza watu wa kawaida wasiwe na Biblia. Tafsiri za Wakatoliki zilizopatikana zilikuwa zenye gharama kubwa, na ni nyumba chache zilizokuwa nazo. Biblia New World Translation of the Christian Greek Scriptures ilitolewa katika Kifaransa mwaka 1963, ikifuatwa na Biblia yote katika 1974. Kufikia 1992 jumla ya pamoja ya nakala 2,437,711 za New World Translation zilikuwa zimesafirishwa ili zigawanywe katika Ufaransa; na idadi ya Mashahidi wa Yehova katika Ufaransa ikaongezeka kwa asilimia 488 wakati wa kipindi hichohicho, kufikia jumla ya 119,674.
Hali ilikuwa iyo hiyo katika Italia. Kwa muda mrefu watu walikuwa wamekatazwa kuwa na nakala ya Biblia. Baada ya kutolewa kwa chapa ya Kiitalia ya New World Translation hadi kufikia 1992, kulikuwa na nakala 3,597,220 zilizogawanywa; nyingi zazo zikiwa Biblia kamili. Watu walitaka kujichunguzia wenyewe yale yaliyomo katika Neno la Mungu. Kwa kupendeza, wakati wa kipindi hichohicho, idadi ya Mashahidi wa Yehova katika Italia ilipanda sana—kutoka 7,801 hadi 194,013.
Wakati New World Translation of the Christian Greek Scriptures ilipotolewa katika Kireno, kulikuwa na Mashahidi 30,118 tu katika Brazili na 1,798 katika Ureno. Wakati wa miaka iliyofuata, hadi kufikia 1992, jumla ya nakala 213,438 za Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo na nakala 4,153,738 za Biblia kamili katika Kireno zilipelekwa kwa watu mmoja-mmoja na makutaniko katika nchi hizo. Matokeo yalikuwa nini? Katika Brazili, wasifaji wa Yehova waliongezeka wakawa mara 11 zaidi; na katika Ureno, wakawa mara 22 zaidi. Makumi ya maelfu ya watu ambao hawakuwa wamepata kuwa na Biblia walishukuru kupata moja, na wengine walithamini kuwa na Biblia iliyotumia maneno ambayo wangeweza kuelewa. Wakati New World Translation of the Holy Scriptures—With References ilipotolewa katika Brazili, vyombo vya habari vilisema kwamba hiyo ilikuwa tafsiri iliyo kamili zaidi (yaani, yenye marejezo-vitomeo na vielezi-chini vingi) iliyopatikana nchini. Pia ilisema kwamba uchapaji wa kwanza ulikuwa mkubwa mara kumi zaidi ya chapa nyingi za kitaifa.
Chapa ya Kihispania ya New World Translation of the Christian Greek Scriptures ilitolewa pia katika 1963, ikifuatwa na Biblia kamili katika 1967. Kulikuwa na nakala 527,451 za Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo zilizochapwa, na baadaye, hadi kufikia 1992, jumla ya nakala 17,445,782 za Biblia kamili katika Kihispania. Hiyo ilitokeza ongezeko lenye kutazamisha la idadi ya wasifaji wa Yehova katika nchi zinazosema Kihispania. Hivyo, kuanzia 1963 hadi 1992, katika nchi ambazo watu wengi husema Kihispania ambapo Mashahidi wa Yehova huendelea na huduma yao, idadi zao zilikua kutoka 82,106 hadi 942,551. Na katika Marekani, mwaka 1992, kulikuwa na Mashahidi wa Yehova wengineo kama 130,224 wenye kusema Kihispania.
Haikuwa katika milki za Jumuiya ya Wakristo tu ambako New World Translation ilipokewa kwa idili. Katika mwaka wa kwanza wa kuchapwa kwa chapa ya Kijapani, ofisi ya tawi ya Japani ilipokea maagizo ya nakala nusu milioni.
-
-
Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu MwenyeweMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Grafu katika ukurasa wa 613]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Ukuzi wa Mashahidi Tangu Kutangazwa kwa “New World Translation”
Ufaransa
150,000
100,000
50,000
1963 1970 1980 1992
Italia
150,000
100,000
50,000
1963 1970 1980 1992
Ureno na Brazili
300,000
200,000
100,000
1963 1970 1980 1992
Nchi Zenye Kusema Kihispania
900,000
600,000
300,000
1963 1970 1980 1992
-