-
Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu MwenyeweMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Ikiwa sehemu ya jitihada nyingi za New World Bible Translation Committee ili kusaidia wapendao Neno la Mungu kujua sana yaliyomo katika maandiko ya Koine ya awali (Kigiriki cha kawaida) ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, halmashauri hiyo ilitokeza The Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures. Hiyo ilitangazwa kwanza na Watch Tower Society katika 1969 na kisha ikatiwa habari za kisasa katika 1985. Ina The New Testament in the Original Greek, kama ilivyotungwa na B. F. Westcott na F. J. A. Hort. Upande wa kulia wa ukurasa huo kuna maandiko ya New World Translation (chapa ya 1984 iliyosahihishwa na kutiwa habari za sasa). Lakini, kati ya mistari ya maandiko ya Kigiriki, kuna tafsiri nyingine, fasili iliyo halisi sana, ya neno kwa neno ya yale ambayo Kigiriki husema hasa kulingana na maana ya msingi na aina ya sarufi ya kila neno. Hilo huwawezesha hata wanafunzi ambao hawawezi kusoma Kigiriki wapate kujua yale hasa yaliyoko katika maandiko ya awali ya Kigiriki.
-
-
Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu MwenyeweMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 610]
“Maandiko Yenye Msamiati wa Hapohapo”
Katika “The Classical Journal,” Thomas N. Winter wa Chuo Kikuu cha Nebraska aliandika pitio la “The Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures” ambayo alisema: “Hiyo ni tafsiri ya mistari kati ya mistari isiyo ya kawaida: uaminifu-maadili wa maandiko unadumishwa, na Kiingereza kinachotokea chini yayo ni maana ya neno la Kigiriki kimsingi. Hivyo sehemu ya mistari kati ya mistari ya kitabu hicho si tafsiri hata kidogo. Maandiko yenye msamiati wa hapohapo waieleza tafsiri hiyo kwa usahihi zaidi. Tafsiri katika Kiingereza safi hutokea katika safu nyembamba kwenye pambizo la upande wa kulia wa kurasa. . . .
“Maandiko hayo yanategemea yale ya Brooke F. Westcott na Fenton J. A. Hort (1881, iliyotokezwa tena), lakini tafsiri iliyofanywa na halmashauri isiyojitambulisha ni ya kisasa kabisa na sahihi kwa upatani.”—Toleo la Aprili-Mei la 1974, kur. 375-376.
[Picha]
Chapa za 1969 na 1985
-