Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwaka wa 1936, Konrad Flatøy, aliyekuwa mchochea-makaa katika merikebu moja, alimpa mfanyakazi mwenzake kijitabu. Mfanyakazi huyo, Paul Bruun, alikubali kijitabu hicho na kukisoma usiku huohuo.

      Paul alisema: “Mara moja niligundua kwamba hii ndiyo kweli, na kijitabu hicho kilinionyesha tofauti kati ya dini ya kweli na ya uwongo.” Kadiri Paul alivyoendelea kujifunza zaidi, ndivyo alivyoanza kuwahubiria wengine. Wakati wa vita, alimfunza Biblia baharia mmoja aliyependezwa na kweli. Baharia huyo alipoendelea kupata ujuzi zaidi, aliamua kwamba hatatumia bunduki zilizokuwa ndani ya merikebu. Wenye mamlaka walipopata kujua msimamo wake, walimwamuru Paul aache kumfundisha Biblia. Paul alikataa na kwa sababu hiyo, yeye na baharia huyo wakaachwa katika pwani ya London. Mwezi mmoja baadaye, merikebu hiyo iligongwa na kombora la chini ya maji na ikazama. Baadaye, baharia huyo alibatizwa, naye Paul akaalikwa kuhudhuria Shule ya Gileadi. Alipohitimu mwaka wa 1954, akatumwa atumike akiwa mmishonari nchini Ufilipino.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 139]

      Paul Bruun

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki