Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kjell Husby, aliyekuwa anatumika Betheli wakati huo, alisema kwamba nyakati zote ofisi ya tawi ilijua mahali ambapo Svanhild alikuwa hasa kwa sababu ya anwani za maandikisho aliyotuma.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukuras wa 132]

      Kuhubiri Katika Sehemu Tambarare

      RANDI HUSBY

      ALIZALIWA 1922

      ALIBATIZWA 1946

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Amekuwa katika utumishi wa wakati wote tangu 1946.

      ◼ WAZAZI wa Randi walibatizwa na kuwa Mashahidi wa Yehova katika mwaka 1938 na baadaye, Randi akaamua kumtumikia Yehova. Mwaka 1946, alikubali mwaliko wa kutumika Betheli, na huko akakutana na ndugu mmoja kijana aliyeitwa Kjell Husby. Randi na Kjell wakachumbiana, wakaoana, na kuanza utumishi wa upainia. Walifurahia kushiriki utendaji mbalimbali wa kiroho katika utumishi wa wakati wote hadi kifo cha Kjell mwaka wa 2010.

      Katika miaka ya hivi karibuni, matatizo ya miguu yamefanya iwe vigumu kwa Randi kupanda ngazi au sehemu zenye mwinuko. Lakini anaweza kutembea vizuri katika sehemu iliyo tambarare naye huonekana mara nyingi akihubiri barabarani na madukani huko Trondheim. Ili kuwahubiria habari njema wote anaokutana nao, Randi huhakikisha amebeba machapisho katika lugha zisizopungua nane. Pia, rafiki za Randi kutanikoni humbeba kwa gari na kumpeleka kwa watu ambao hupokea magazeti ya karibuni kutoka kwake kwa ukawaida.

      Randi hana nguvu za kufanya mengi kama alivyofanya hapo zamani. Lakini anaendelea kupata shangwe na uradhi kutokana na utumishi wake wa nafsi yote, akijua kwamba Yehova ‘hatasahau kazi yake na upendo alioonyesha kwa ajili ya jina lake.’—Ebr. 6:10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki