Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MASHUA ZASAIDIA KUKUSANYA UMATI MKUBWA

      Kazi ya kuhubiri ilipoanza nchini Norway, ilionekana kwamba ingekuwa vigumu kuwafikia watu walioishi kwenye visiwa vingi sana vya nchi hiyo, na maeneo mengine ya pwani yaliyo mbali. Hivyo, mnamo 1928, ofisi ya tawi ilinunua mashua yenye injini, ambayo ingewatosha mapainia wawili au watatu na yenye nguvu inayoweza kuabiri pwani ya Norway iliyochongoka sana. Lakini nani angekuwa nahodha wa mashua hiyo? Karl Gunberg, painia mwenye uzoefu alijitolea. Ujuzi wake alipokuwa katika jeshi la wanamaji na pia akiwa mwalimu wa mambo ya usafiri ulimsaidia sana. Mashua ya kwanza iliyoitwa Elihu, ilianza safari huko Oslo, ikaelekea kaskazini huku ikitia nanga katika bandari mbalimbali. Hata hivyo, usiku mmoja wa majira ya baridi kali ya mwaka wa 1929, kulitokea dhoruba kubwa iliyoiharibu mashua hiyo karibu na Stavanger. Wote walishukuru kwamba ndugu katika mashua hiyo walifika ufuoni salama.

      Mnamo 1931 ndugu walipata mashua nyingine waliyoiita Ester. Kwa mara nyingine tena, Karl akashika usukani akisaidiwa na ndugu wengine wawili. Ester ilitumiwa magharibi na kaskazini mwa Norway kwa miaka saba iliyofuata. Mwaka wa1932, Karl alihisi kwamba “amezeeka na hivyo hawezi kuendelea na safari hizo.” Kwa hiyo, akamwachia Johannes Kårstad usukani na akatumika akiwa painia katika eneo la mashariki mwa Norway. Mwaka wa 1938, mashua iliyoitwa Ruth ilichukua mahali pa Ester na ikatumiwa mpaka 1940, wakati kazi ya kuhubiri kwa mashua ilipokoma kwa sababu ya Vita vya Pili vya Ulimwengu. Wahubiri hao wa kutumia mashua walihubiri maeneo mengi na kuwaachia watu machapisho mengi. Katika mwaka wa 1939, Andreas Hope na Magnus Randal waliotumia mashua Ruth, waliripoti kwamba kwa mwaka mmoja tu, waliwaachia watu zaidi ya vitabu 16,000, vijitabu, magazeti, na watu 2,531 wakasikiliza hotuba kwenye gramafoni mara 1,072.

      Kando na matokeo mazuri ya kiroho, ndugu hao pia waliona mandhari zenye kupendeza. Andreas Hope alisema, “Kila siku tulielekea kaskazini tukiingia na kutoka ndani ya mikono-bahari na kuzunguka rasi refu. Mandhari ilikuwa maridadi sana.” Wakati wa majira ya baridi kali, wakiwa upande wa kaskazini ya Mzingo wa Aktiki waliona “uzuri wa ajabu wa mianga ya kaskazini [aurora borealis].” Na wakati wa kiangazi, waliduwazwa na “uangavu wa jua la usiku wa manane.”

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sandku/Picha katika ukurasa wa 113]

      Alitimiza Ahadi Yake

      JOHANNES KÅRSTAD

      ALIZALIWA 1903

      ALIBATIZWA 1931

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Alitumika katika mashua za mapainia kwa miaka minane.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kuanzia 1931 hadi 1938, alitumia mashua ya mapainia inayoitwa Ester, na kisha akafanya upainia kwa mwaka mmoja hivi akitumia mashua Ruth, akisafiri kandokando ya pwani kuelekea upande wa kaskazini hadi Tromsø.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 114]

      Karl Gunberg alikuwa nahodha wa mashua iliyoitwa “Elihu”

      [Picha katika ukurasa wa 115]

      Johannes Kårstad alikuwa nahodha wa mashua iliyoitwa “Ester”

      [Picha katika ukurasa wa 116]

      Andreas Hope na Magnus Randal walitumika katika mashua iliyoitwa “Ruth”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki