Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Gestapo walimkamata Andreas Kvinge huko Bodø Julai 1941 na kumwuliza mahali walikokuwa Mashahidi wa kaskazini mwa Norway. Andreas alijibu kwa unyoofu, “Sijui wako wapi leo.” Wazia jinsi Andreas alivyohisi wakati maofisa hao walipotawanya sakafuni vitu vilivyokuwa mkobani mwake, yaani, karatasi zenye orodha ya majina na anwani za makutaniko, watumishi wa makutaniko, na watu wanaopendezwa. Jambo la kupendeza ni kwamba, hakuna ofisa hata mmoja aliyejishughulisha kusoma karatasi hizo. Tamaa yao kubwa ilikuwa ni kumfanya Andreas atie sahihi taarifa ya kukubali marufuku dhidi ya Mashahidi wa Yehova na kazi ya kuhubiri.

      Andreas aliwaambia, “Tunajua kwamba kazi yetu imepigwa marufuku, kwa hiyo ninaweza kutia sahihi taarifa hii. Lakini, hata mkitukataza kufanya mikutano na kuwapa watu magazeti na vitabu, tutaendelea kuwaeleza watu kuhusu Ufalme wa Mungu tukitumia Biblia.” Hatimaye, Gestapo walimwachilia Andreas walipoona kwamba hatalegeza msimamo wake.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mnamo 1943, Magnus Randal, ambaye awali alitumia mashua Ruth, alipata anwani kadhaa kutoka kwa Ndugu Öman na kuelekea kaskazini kwa baiskeli, umbali wa kilomita 1,200, mpaka Bodø ili kuwatia moyo ndugu na dada.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki