Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Meli ilipokaribia pwani, Knud alitazama kwa makini nchi hii maridadi—nchi nyembamba yenye milima mirefu iliyofunikwa kwa theluji, mikono-bahari yenye kupendeza na misitu mikubwa. Alitambua kwamba haingekuwa rahisi kufikia maeneo yenye watu wachache sana na ambayo yalikuwa na madaraja na barabara chache tu. Ingawa watu wengi wa Norway waliishi katika miji iliyokuwa ikipanuka siku baada ya siku, wengine waliishi katika maeneo ya mashambani, vijiji vya wavuvi, au katika visiwa vingi katika pwani ya Norway.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 90]

      Maelezo Mafupi Kuhusu Norway

      Nchi

      Norway inajulikana kwa mikono-bahari maridadi na milima yenye kustaajabisha na vilevile maelfu ya visiwa. Bila kuhesabu visiwa vya Svalbard vilivyo katikati ya Norway barani na Ncha ya Kaskazini, nchi hiyo ni kubwa kidogo kuliko Italia. Ingawa kunaweza kuwa na baridi kali nchini Norway, hasa katika eneo la Aktiki, sehemu kubwa ya nchi hii ina joto la kadiri ikilinganishwa na nchi nyingine zilizo katika maeneo kama hayo kwa sababu ya mawimbi yenye joto na mfumo upepo kutoka bahari ya Atlantiki.

      Watu

      Wengi wa wakaaji milioni tano ni wenyeji wa Norway, na asilimia 10 hivi ni wahamiaji. Wasami (waliojulikana kama Lapp) bado wanajitegemeza kwa kuvua samaki, kuwinda na vilevile kufuga mbawala.

      Lugha

      Kinorway ndiyo lugha rasmi na huandikwa kwa njia mbili—Nynorsk, na Bokmål inayotumiwa na watu wengi sana na inakaribiana na Kidenishi.

      Kazi

      Viwanda vya mafuta na gesi ndio vyanzo vikuu vya mapato nchini. Samaki huuzwa katika nchi za nje kwa wingi. Ni asilimia 3 tu ya ardhi nchini Norway inayotumiwa kukuza mimea.

      Chakula

      Samaki, nyama, viazi, mkate, na mazao ya maziwa ni vyakula vya kawaida nchini Norway. Chakula kinachopendwa sana ni Fårikål (mchuzi wa nyama ya kondoo na kabichi). Kwa sababu ya ongezeko la wahamiaji katika miaka ya karibuni, chakula hicho sasa kinapendwa hata na watu wa mataifa mengine.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki