Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mnamo Septemba 1945, Nathan H. Knorr, wa makao makuu aliwasiliana na Marvin F. Anderson, Mmarekani mwenye asili ya Denmark, aliyekuwa na umri wa miaka 28. Awali Anderson alitumika Betheli ya New York lakini wakati huo alikuwa mwangalizi wa mzunguko nchini Marekani. Ndugu Knorr alimwuliza Ndugu Anderson kama angekubali kwenda Norway kushughulikia mambo fulani na kuishi huko “kwa miaka kadhaa.” Anderson alikubali, ijapokuwa angefika huko baada ya miezi kadhaa.

      Hata hivyo, Ndugu Knorr na Ndugu Henschel walienda Norway mnamo Desemba 1945. Mwongozo waliotoa kwa upendo uliwasaidia ndugu kupendana zaidi na kudumisha umoja. Wakati huohuo, Ndugu Knorr alitangaza kuwa Ndugu Dey angechukua mahali pa Ndugu Öman kama msimamizi wa tawi. Mwezi mmoja baadaye, Ndugu Anderson aliwasili, na akawekwa rasmi kuwa msimamizi wa tawi mwezi wa Februari.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kufikia wakati ambapo Marvin Anderson alifika Norway, ofisi ya tawi ilikuwa na utendaji mwingi.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu Anderson alipowekwa kuwa mwangalizi wa tawi mwaka wa 1946, ofisi ya tawi ilikuwa ndogo sana, hivyo aliishi katika chumba kimoja na ndugu wengine watano. Wakaaji wasio Mashahidi waliokuwa wakiishi katika jengo hilo tangu enzi za Nazi walihamishwa ili kupata nafasi kwa ajili ya familia ya Betheli iliyokuwa ikiongezeka.

      Ndugu Anderson alikuwa na bidii sana katika mgawo wake mpya. Jengo la ofisi lilifanyiwa marekebisho na vifaa vipya vikanunuliwa, kutia ndani matbaa inayoendeshwa kwa mguu.

  • Norway
    2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 127]

      Marvin Anderson na mke wake, Karen

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki