-
Norway2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mazoezi ambayo wamishonari hupata katika Shule ya Gileadi huko New York yamewasaidia sana akina ndugu nchini Norway. Hans Peter Hemstad na Gunnar Marcussen, waliohitimu kutoka Gileadi mwaka wa 1948, walikuwa wanafunzi wa kwanza kutoka Norway. Walitumwa Norway na kutumika katika kazi ya kuzungukia makutaniko na pia Betheli, mwanzoni wakiwa waseja na baadaye wakiwa pamoja na wake zao. Tangu 1948 hadi 2010, wahubiri 45 hivi kutoka Norway walihitimu kutoka Shule ya Gileadi. Zaidi ya nusu yao walitumwa Norway na wametumikia wakiwa wahubiri wa wakati wote au waangalizi wanaosafiri au washiriki wa familia ya Betheli.
-
-
Norway2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 135]
Gunnar Marcussen (1) na Hans Peter Hemstad (2) walikuwa wanafunzi wa kwanza kutoka Norway kuhitimu Shule ya Gileadi
-