-
Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?Amkeni!—2004 | Machi 8
-
-
Washiriki Wapya wa Chama cha Nyuklia
Ijapokuwa silaha nyingi za nyuklia zinamilikiwa na mataifa mawili yenye nguvu, kuna mataifa mengine yenye silaha za nyuklia kama vile China, Ufaransa, na Uingereza. Mataifa hayo yanaitwa chama cha nyuklia, na hivi majuzi India na Pakistan zimekuwa wanachama. Mbali na nchi hizo, nchi nyingine kadhaa, kutia ndani Israel, mara nyingi huonwa kuwa zinataka kuunda au tayari zina silaha hizo.
Migogoro ya kisiasa kati ya washiriki wa chama cha nyuklia, kutia ndani wanachama hao wapya, inaweza kuchochea vita vya nyuklia. Gazeti Bulletin of the Atomic Scientists linasema kwamba “mgogoro kati ya India na Pakistan . . . ni mfano wa jinsi mataifa mawili yalivyokaribia vita vya nyuklia zaidi tangu Mgogoro wa Makombora wa Kuba.” Watu wengi walianza kuogopa sana kwamba vita vya nyuklia vingetokea wakati hali zilipochacha mapema mwaka wa 2002.
-
-
Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?Amkeni!—2004 | Machi 8
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 6]
Je, Hii Ni Enzi ya Pili ya Nyuklia?
Akiandika katika gazeti The New York Times Magazine, mwandishi Bill Keller (ambaye sasa ni mhariri mkuu wa gazeti The New York Times) alisema kwamba mataifa yako katika enzi ya pili ya nyuklia. Enzi ya kwanza iliisha Januari 1994, wakati nchi ya Ukrainia ilipokubali kusalimisha silaha ilizorithi kutoka kwa ule uliokuwa Muungano wa Sovieti. Kwa nini anasema kuhusu enzi ya pili ya nyuklia?
Keller anaandika hivi: “Enzi ya pili ya nyuklia ilianza kwa kishindo katika jangwa la Rajasthani mwaka wa 1998, wakati serikali mpya ya India ilipolipua mabomu matano ya majaribio. Majuma mawili baadaye Pakistan ikafanya vivyo hivyo.” Ni nini kilichofanya majaribio hayo kuwa tofauti na ya enzi ya kwanza ya nyuklia? “Hizo zilikuwa silaha za nyuklia zilizokusudiwa kutumiwa katika eneo hususa.”
Kwa hiyo, je, ulimwengu unaweza kuwa salama ikiwa kuna nchi mbili mpya zenye silaha za nyuklia? Keller anaongezea hivi: “Kila nchi inayopata silaha za nyuklia inaongeza uwezekano wa vita vinavyohusisha taifa lenye silaha za nyuklia.” —“The Thinkable,” The New York Times Magazine, Mei 4, 2003, ukurasa wa 50.
Hali hiyo inakuwa mbaya zaidi kutokana na habari kwamba huenda Korea Kaskazini ina “kiasi cha kutosha cha plutoniamu inayoweza kutengeneza mabomu sita mapya ya nyuklia. . . . Kila siku kuna hofu zaidi kwamba Korea Kaskazini itafaulu kutengeneza silaha mpya za nyuklia na hata labda kujaribu kutumia mojawapo ili kuonyesha imefaulu.” —The New York Times, Julai 18, 2003.
-