Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutia Muhuri Israeli wa Mungu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ni Wangapi Wanatiwa Muhuri

      10. (a) Ni maandiko gani yanaonyesha kwamba hesabu ya watiwa muhuri ina kikomo? (b) Ni nini jumla ya hesabu iliyotiwa muhuri, na wao wanaorodheshwaje?

      10 Yesu aliambia wale waliokuwa katika mstari wa huku kutiwa muhuri: “Msiwe na hofu, kundi dogo, kwa sababu Baba yenu ametoa kibali cha kuwapa nyinyi ufalme.” (Luka 12:32, NW) Maandiko mengine, kama vile Ufunuo 6:11 na Warumi 11:25, huonyesha kwamba hesabu ya hili kundi dogo ina kikomo kweli kweli na, kwa hakika, ilikusudiwa kimbele. Maneno ya Yohana yanayofuata yanathibitisha hili: “Na mimi nikasikia hesabu ya wale ambao walitiwa muhuri, mia na arobaini na nne elfu, waliotiwa muhuri kutoka kila kabila la wana wa Israeli: Kutoka kabila la Yuda elfu kumi na mbili walitiwa muhuri; kutoka kabila la Reubeni elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Gadi elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Asheri elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Naftali elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Manase elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Simeoni elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Lawi elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Isakari elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Zebuloni elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Yosefu elfu kumi na mbili; kutoka kabila la Benyamini elfu kumi na mbili walitiwa muhuri.”—Ufunuo 7:4-8, NW.

      11. (a) Ni kwa nini lile rejezo kwa makabila 12 halingeweza kutumika kuhusu Israeli halisi, wa mnofu? (b) Ni kwa nini Ufunuo huorodhesha makabila 12? (c) Ni kwa nini hakuna kabila ambalo hilo pekee ndilo la kifalme au la kikuhani katika Israeli wa Mungu?

      11 Je! hii haingeweza kuwa inarejeza kwa Israeli halisi, wa mnofu? La, kwa kuwa Ufunuo 7:4-8 hutofautiana na ile orodha ya kawaida ya kikabila. (Hesabu 1:17, 47) Kwa wazi, orodha hii hapa si kwa kusudi la kutambulisha Wayahudi wa mnofu kwa makabila yao bali ni kuonyesha muundo wa kitengenezo kama huo kwa Israeli wa kiroho. Hili linasawazika. Wanapaswa waweko washiriki 144,000 wa hili taifa jipya—12,000 kutoka kila mojapo makabila 12. Hakuna kabila katika huyu Israeli wa Mungu ambalo hilo pekee ndilo la kifalme au la kikuhani. Taifa lote kwa ujumla litatawala likiwa wafalme, na taifa lote kwa ujumla litatawala likiwa makuhani.—Wagalatia 6:16; Ufunuo 20:4, 6.

  • Kutia Muhuri Israeli wa Mungu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 14. Ni nini linaloonyesha kwamba bila ugeugeu Mashahidi wa Yehova wameshikilia kwamba 144,000 ni hesabu halisi ya wale wanaojumlika kuwa Israeli wa kiroho?

      14 Kwa kupendeza, Charles T. Russell, alitambua 144,000 kuwa hesabu halisi ya watu mmoja mmoja wanaojumlika kuwa Israeli wa kiroho. Katika The New Creation, Buku 6 la mfululizo wake wa Studies in the Scriptures, kilichotangazwa 1904, yeye aliandika: “Sisi tuna kila sababu kuitikadi kwamba ile hesabu dhahiri, iliyo imara ya wateule [wapakwa-mafuta waliochaguliwa] ni ile ambayo imetaarifiwa mara kadhaa katika Ufunuo (7:4; 14:1); yaani, 144,000 ‘waliokombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu.’” Katika Light, Kitabu cha Kwanza, kilichotangazwa katika 1930 na Wanafunzi wa Biblia, ilitaarifiwa hali kadhalika hivi: “Hivyo washiriki 144,000 wa mwili wa Kristo wako katika kusanyiko wakionyeshwa kuwa wamechaguliwa na kupakwa mafuta, au kutiwa muhuri.” Bila ugeugeu Mashahidi wa Yehova wameshikilia oni la kwamba kihalisi Wakristo wapakwa-mafuta 144,000 wanajumlika kuwa Israeli wa kiroho.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki