Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Aja na Kitia-Moyo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 2. (a) Nambari “saba” inamaanisha nini? (b) Katika kipindi cha siku ya Bwana, zile jumbe kwa yale “makundi saba” zinahusu akina nani?

      2 Hapa Yohana anasema kwa “makundi saba,” na hayo yanapewa majina kwa ajili yetu baadaye katika unabii huu. Nambari hiyo, “saba,” inarudiwa mara nyingi katika Ufunuo. Inamaanisha ukamilifu, hasa kuhusiana na mambo ya Mungu na kundi lake lililopakwa mafuta. Kwa kuwa hesabu ya makundi ya watu wa Mungu ulimwenguni pote imeongezeka kufika makumi ya maelfu katika kipindi cha siku ya Bwana, sisi tunaweza kuwa na uhakika kwamba yanayosemwa kwanza kabisa kwa yale “makundi saba” ya wapakwa-mafuta yanahusu pia watu wote wa Mungu leo. (Ufunuo 1:10, NW)

  • Yesu Aja na Kitia-Moyo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Vilevile, zinazohusika hapa ni “zile roho saba,” usemi ambao unaonyesha utendaji kamili wa kani-tendaji ya Mungu, au roho takatifu, inapoleta uelewevu na baraka kwa wote wanaoupa unabii huu uangalifu.

  • Yesu Aja na Kitia-Moyo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Chati katika ukurasa wa 19]

      Nambari za Mfano Katika Ufunuo

      Nambari Maana ya Mfano

      2 Humaanisha kuthibitisha kiimara jambo fulani.

      (Ufunuo 11:2, 4; linga Kumbukumbu 17:6.)

      3 Huonyesha mkazo. Huonyesha pia wingi.

      (Ufunuo 4:8; 8:13; 16:13, 19)

      4 Humaanisha mweneo wa kotekote au upembenne

      kwa ulingano. (Ufunuo 4:6; 7:1, 2; 9:14; 20:8; 21:16)

      6 Humaanisha kutokamilika, kitu kisicho cha kawaida,

      cha dubwana. (Ufunuo 13:18; linga 2 Samweli 21:20.)

      7 Humaanisha ukamili ulioyakinishwa kimungu, wa

      makusudi ya Yehova au yale ya Shetani.

      (Ufunuo 1:4, 12, 16; 4:5; 5:1, 6; 10:3, 4; 12:3)

      10 Humaanisha uwote au ukamili kimwili, wa vitu duniani.

      (Ufunuo 2:10; 12:3; 13:1; 17:3, 12, 16)

      12 Humaanisha tengenezo lililofanyizwa kimungu

      ama katika mbingu ama katika dunia.

      (Ufunuo 7:5-8; 12:1; 21:12, 16; 22:2)

      24 Humaanisha mpango tele (uliorudufiwa) wa kitengenezo

      wa Yehova. (Ufunuo 4:4)

      Nambari nyingine zinazotajwa katika Ufunuo zapasa kueleweka kihalisi. Mara nyingi, muktadha husaidia kuyakinisha hili. (Ona Ufunuo 7:4, 9; 11:2, 3; 12:6, 14; 17:3, 9-11; 20:3-5.)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki