Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutafuta Matabiri Yanayotumainika
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
    • Kutafuta Matabiri Yanayotumainika

      PUNDE baada ya kuanza kutawala mwaka wa 336 K.W.K., Mfalme wa Makedonia aliyekuja kuitwa Aleksanda Mkuu alizuru madhabahu ya uaguzi ya Delphi huko Ugiriki ya kati. Katika mipango yake ya wakati ujao, yeye alikuwa na lengo la kushinda sehemu kubwa ya ulimwengu wa wakati huo. Lakini alitaka uhakikisho wa kimungu kwamba angefanikiwa katika shughuli hiyo kubwa. Hekaya husema kwamba siku ambapo alizuru Delphi, haikuruhusika kuwasiliana na mwaguzi wa madhabahu hiyo. Kwa kuwa hakutaka kuondoka bila jibu, Aleksanda alisisitiza, akimlazimisha kuhani huyo wa kike kutabiri. Kwa kukata tamaa, alisema hivi kwa sauti kubwa: “Ee, mtoto, hushindiki!” Mfalme huyo mchanga alichukua maneno hayo kuwa ishara ya mema—iliyotoa ahadi ya ushindi katika kampeni yake ya kijeshi.

  • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
    • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia

      MFALME PIRO wa Epirus, kaskazini-magharibi mwa Ugiriki, alipambana kwa muda mrefu na Milki ya Roma. Akitaka sana kupata habari yenye kutegemeka kuhusu matokeo ya pambano hilo, alienda kutafuta habari katika madhabahu ya uaguzi ya Delphi. Lakini jibu alilopata lingeweza kueleweka katika mojawapo ya njia hizi mbili: (1) “Nasema kwamba wewe mwana wa Æacus unaweza kuwashinda Waroma. Wewe utaenda, wewe utarudi, hutaangamia vitani kamwe.” (2) “Nasema kwamba Waroma wanaweza kukushinda wewe, mwana wa Æacus. Wewe utaenda, wewe hutarudi, utaangamia vitani.” Aliamua kuelewa habari zilizotolewa katika sehemu ya kwanza ya jibu hilo, hivyo akafanya vita dhidi ya Roma. Piro alishindwa kabisa.

  • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
    • Habari za waaguzi zilitambuliwa kwa kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa mfano, mjini Delphi majibu yalitolewa kwa sauti zisizoeleweka. Hilo lilifanya iwe lazima kwa makuhani kuzifasiri na kubuni mistari ambayo ingeweza kutoa fasiri zilizo tofauti kabisa. Jibu lililopewa Croesus, mfalme wa Lidia, ni mfano halisi. Alipotafuta habari kwenye madhabahu ya uaguzi, aliambiwa hivi: “Croesus akivuka Halys, ataharibu milki yenye nguvu.” Kwa kweli, “milki yenye nguvu” iliyoharibiwa ilikuwa yake mwenyewe! Wakati Croesus alipovuka mto Halys ili kushambulia Kapadokia, alishindwa na Koreshi Mwajemi.

  • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
    • MADHABAHU YA UAGUZI YA DELPHI ndiyo yaliyokuwa maarufu zaidi katika Ugiriki ya Kale.

      Mivuke yenye kulevya iliyotoka kwenye tundu hili ilimfanya nabii huyo wa kike afikie upeo wa shangwe

      [Picha]

      Kuhani wa kike aliagua akiwa ameketi juu ya kigoda hiki

      Sauti alizotoa ziliaminika kuwa na ufunuo mbalimbali kutoka kwa mungu Apolo

  • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
    • Matabiri yaliyotolewa kwenye madhabahu ya uaguzi ya Delphi hayakuwa yenye kutegemeka hata kidogo

      [Hisani]

      Delphi, Ugiriki

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki