Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ninapenda Muziki, Maisha, na Biblia
    Amkeni!—2007 | Agosti
    • Okestra ya Filimbi

      Niliendeleza masomo yangu ya muziki na nikawa nautumia kujipatia riziki. Baada ya kujifunza kupiga ala mbalimbali za muziki, nilijifunza kupiga filimbi. Wakati mmoja, nilirekebisha filimbi ndogo iliyotengenezwa kwa mianzi. Muda si muda, nilijifunza kutengeneza filimbi zangu mwenyewe. Wakati huo, wataalamu walifikiri haiwezekani kutengeneza filimbi zinazotoa sauti nzito kwani filimbi zilikuwa kubwa sana na hivyo sauti iliyotokezwa ilikuwa ya chini sana. Hiyo ndiyo sababu hakukuwa na okestra za filimbi.

      Hata hivyo, nilifaulu kutengeneza filimbi yenye kifaa cha kuongezea mvumo, au sauti. Hilo lilimaanisha kwamba filimbi zenye sauti nzito zingeweza kutengenezwa. Baada ya muda, nilianza kutengeneza filimbi ambazo zingepigwa kwa mfuatano ili kutoa viwango mbalimbali vya sauti nzito.

      Kabla ya hapo nilikuwa nimepanga okestra zilizotumia ala za kitamaduni. Mojawapo ya okestra zangu ilikuwa na wanamuziki vipofu peke yao. Mnamo 1960, nilipanga okestra ambayo ilipiga filimbi tu. Hiyo ilikuwa ya kwanza ya aina hiyo katika Muungano wa Sovieti au hata labda ulimwenguni pote.

  • Ninapenda Muziki, Maisha, na Biblia
    Amkeni!—2007 | Agosti
    • Mnamo 1981, baada ya kuishi Kam’yanets’-Podil’s’kyy kwa miaka 35, nilihama na kwenda mji wa Yoshkar-Ola ulio kilomita 600 hivi mashariki mwa Moscow. Nikiwa huko niliendelea na ubunifu wangu. Okestra yangu moja ilikuwa na wanamuziki 45 waliopiga filimbi tofauti-tofauti. Kati ya hizo filimbi, nyingine zilikuwa na urefu wa sentimita 20 na zilitoa sauti nyembamba, nyingine za kipenyo cha sentimita moja, nazo nyingine zenye urefu wa mita tatu na kipenyo cha sentimita 20 na zilitoa sauti nzito. Maonyesho yetu yalitangazwa kwenye redio na kwenye televisheni, pia tulikuwa na maonyesho mengi kotekote nchini.

      Katika mashindano yaliyohusisha vikundi vya muziki kutoka sehemu zote za Muungano wa Sovieti mwaka wa 1986, nilipewa cheti na medali kwa sababu ya kukuza muziki wa filimbi. Miaka mingi baadaye, sinema inayoitwa Solo for Pipe, or the Fairy Tale of a Musician ilitokezwa. Gazeti Mariiskaya Pravda liliripoti hivi: “Boris Nikolaievich Gulashevsky anayezungumziwa katika sinema hii, alipata cheti cha pekee kwa kuanzisha okestra ya filimbi kwa sababu hakuna nyingine kama hiyo nchini Urusi.”

  • Ninapenda Muziki, Maisha, na Biblia
    Amkeni!—2007 | Agosti
    • [Picha katika ukurasa wa 20, 21]

      Okestra ya filimbi

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki