-
Programu ya Elimu Yenye Matokeo MakubwaAmkeni!—2000 | Desemba 22
-
-
Kusini ya Pasifiki, watu wapatao 7,000 huzungumza Kinauru, 4,500 Kitokelau, na 12,000 Kirotuma. Sasa Mashahidi huchapisha trakti za Biblia na broshua katika lugha hizo na vilevile matoleo ya kila mwezi ya Mnara wa Mlinzi katika Kiniue, lugha inayozungumzwa na watu 8,000 hivi, na Kituvalu, kinachozungumzwa na watu wapatao 11,000. Kwa kweli, Mashahidi wa Yehova ni mojawapo wa wachapishaji wakuu zaidi wa vichapo katika lugha zisizojulikana sana, wanachapisha vichapo vya Biblia katika lugha kama vile Kibislama, Kihiri Motu, Kipapiamento, Kikreoli cha Mauritius, Kipijini cha New Guinea, Kikreoli cha Shelisheli, Kipijini cha Visiwa vya Solomon, na lugha nyinginezo nyingi.
-
-
Programu ya Elimu Yenye Matokeo MakubwaAmkeni!—2000 | Desemba 22
-
-
Linda Crowl, mfanyakazi katika Taasisi ya Pacific Studies, iliyo katika Chuo Kikuu cha South Pacific huko Suva, Fiji, alisema kwamba kazi ya kutafsiri ya Mashahidi ndilo “jambo lenye kuvutia zaidi linalofanywa katika Pasifiki.” Anapendekeza vichapo vyao kwa sababu ya ubora wake wa hali ya juu.
Wakati matoleo ya baada ya kila miezi mitatu ya Amkeni! yalipoanza kuchapishwa katika lugha ya Kisamoa, magazeti ya habari vilevile kituo cha taifa cha televisheni kilitangaza habari hizo. Wakati wa matangazo hayo jalada la Amkeni! lilionyeshwa, na kila makala ya gazeti hilo ilionyeshwa. Kisha makala hizo zikazungumziwa moja baada ya nyingine.
-